31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MRUNDI, OFISA NBC MBARONI MAUAJI YA MWANAHARAKATI WA TEMBO

PATRICIA KIMELEMETA NA MANENO SELANYIKA

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewapandisha kizimbani watu watano, akiwamo raia wa Burundi, Ndikumana Jonas (40) na kuwasomea mashtaka mawili, likiwamo la mauaji ya aliyekuwa mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa Taasisi ya Pams Foundation, Wyne Dereck Lotter.

Mbali na raia huyo, washtakiwa wengine ni Godfrey Salamba (42), Innocent Kimara (23), Chambie Ally (32) na Robert Harride (31), ambaye ni Ofisa wa Benki ya NBC.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yanayowakabili na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Yamiko Mlekano, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili Mlekano alidai kuwa, katika kesi hiyo washtakiwa watatu hawapo mahakamani. Katika shtaka la kwanza, wanakabiliwa na shtaka la kutenda njama ya mauaji, tukio lililotokea kati ya Julai Mosi na Agosti 16, mwaka jana, ndani ya Jamhuri ya Muungano, walimuua Wyne Dereck Lotter.

Shtaka la pili wakili huyo alidai Agosti 16, mwaka jana, katika makutano ya Barabara ya Chole na Haile Salasie, Kinondoni, walimuua Wayne Dereck Lotter.

Baada ya maelezo hayo, Wakili Mlekano alidai upelelezi wa kosa hilo bado haujakamilika, hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu alisema washtakiwa hawapaswi kujibu chochote, kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

“Makosa yanayowakabili  hayana dhamana, hivyo upelelezi utakapokamilika kesi yenu itahamishiwa Mahakama Kuu ili ikasikilizwe,” alisema Hakimu Mashauri.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 6, mwaka huu, itakapotajwa na washtakiwa walirudishwa mahakamani.

Lotter (51) aliuawa kwa kile kinachodaiwa kupigwa risasi na watu waliovalia kininja, katika eneo la Masaki, Dar es Salaam Agosti mwaka jana, wakati akielekea katika hoteli moja  akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles