27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

MRITHI WA SIRRO AKABILIWA NA CHANGAMOTO TANO

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo kwa kumteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Juma Yusuf Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, DCP Juma alikuwa ni Mkuu wa Utawala na Fedha, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Hatua ya hiyo inatokana na kustaafu kwa aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza umri wa miaka 60.

 

MRITHI WA SIRRO

Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Barnabas Mwakalukwa, ilieleza kwamba mbali na uteuzi huo, IGP Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambayo ilikuwa ikiongozwa na Sirro kabla ya Mei 28, mwaka huu kuteuliwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi huo, Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Pia aliwahi kuwa RPC wa Mkoa wa Simiyu.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, amepelekwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, huku aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Neema Mwanga akipelekwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

“IGP Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gilles Mroto, kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke.

“Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mbeya,” alisema Mwakalukwa katika taarifa yake.

Mwakalukwa alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja kuendelea kuiweka nchi salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles