26 C
Dar es Salaam
Saturday, February 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mrithi wa Kafulila aingia rasmi ofisini Songwe

Na Mwandishi wetu-Songwe

KATIBU Tawala Mkoa wa Songwe, Dk. Seif Abdallah Shekalaghe, amewasili rasmi katika ofisi za Mkoa wa Songwe na kupokewa na viongozi mbalimbali pamoja na watumishi wa ofisi hiyo.

Dk. Shekalaghe aliteuliwa kushika nafasi ya Kafulila ambaye aligombea ubunge kwenye Jimbo la Kigoma Kusini na kuangushwa kwenye kura za maoni.

Jana mara baada ya mapokezi yake yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangelaa, alizungumza na watumishi wote wa ofisi hiyo na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu huku akiwaeleza kuwa katika utendaji wake hatoweza kumvumilia mtumishi yeyote ambaye si mwadilifu.

“Mtumishi asiye mwadilifu si rafiki yangu, lakini nawahakikishia katika utendaji wangu sitamwonea mtumishi yeyote isipokuwa akitenda maovu na nikipata ushahidi basi sheria itafuata mkondo wake,” alisema Dk. Shekalaghe.

Alisema  anapenda watumishi wote wafanye kazi kwa ushirikiano, umoja, uwazi ,uzalendo, uadilifu na kazi watakazofanya zilete matokeo chanya katika maendeleo ya Mkoa wa Songwe.

Dk. Shekalaghe aliongeza kuwa utendaji kazi wake utakuwa wa kufuata taratibu na sheria zote huku akiahidi kuwathamini watumishi wa ngazi zote kwani anaamini hata mtumishi wa ngazi ya chini anao mchango mkubwa katika maendeleo, hivyo watumishi wawe huru kumwona wanapomuhitaji.

Naye Brigedia Jenerali Mwangela alimkaribisha Dk. Shekalaghe na kumuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akiwataka watumishi wote kumpa ushirikiano wa kutosha bila fitna au matatizo yoyote.

Alisema Rais Dk. John Magufuli amemwamini Dk. Shekalaghe kuwa anao mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya haraka kwa Mkoa wa Songwe, hivyo atumie uzoefu wake katika kuwasaidia wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles