30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mradi wa ‘Wanawake Wanaweza’watambulishwa na TAMWA

Na Asha Bani

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimetambulisha na kuanza mradi wa ‘Wanawake Wanaweza’ unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wanawake (UN-Women).

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Rose Reuben alisema mradi huo una lengo kuu la utetezi wa haki za wanawake na watoto, kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi, kuondoa mifumo kandamizi inayochochea ukatili kwa makundi hayo maalum kwa kutumia vyombo vya habari.

“Katika kufanikisha lengo kuu la mradi huo, TAMWA itawajengea uwezo wanahabari katika kuripoti habari za jinsia na ufuatiliaji wa ushiriki wa wanawake katika uongozi na siasa, ” alisema Rose.

Pia TAMWA itaendesha midahalo katika mikoa 16 ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma , Singida , Tabora na Shinyanga, Mwanza , Mara , Mbeya, Ruvuma , Lindi na Mtwara .

Pia wilaya 112 za mikoa hiyo na kata 48 ndio maeneo yatakayotumika kama sampuli ya utekelezaji wa mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles