25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MRADI WA UMEME WA MEGAWATI 80 KUZINDULIWA LEO

Na MWANDISHI WETU, NGARA

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, leo anatarajia kuzindua mradi wa kuzalisha umeme wa nishati ya maji wa megawati 80 utakaohudumia nchi tatu za Afrika Mashariki katika eneo la Rusumo, Mto Kagera.

Uzinduzi wa mradi huo ambao utashuhudiwa pia na mawaziri kutoka nchi za Rwanda na Burundi, unalenga kusaidia kaya zaidi ya 7,000.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na wasimamizi wa mradi huo ambao ni Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program Coordination Unit (NELSAP-CU), utanufaisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.

“Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha kaya 7,000 kupitia mpango wa maendeleo katika Serikali za Mitaa na kaya nyingine 188 zinazozunguka mradi huu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme unagharimiwa na Benki ya Dunia wakati ujenzi wa njia ya umeme kuuunganisha katika gridi za Taifa za nchi hizo tatu, unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Taarifa hiyo iliwataja wadau wengine wanaotarajiwa katika uzinduzi huo kuwa ni wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, AfDB pamoja na wajumbe wa bodi ya mradi wa umeme wa Rusumo kutoka nchi hizo tatu wanachama.

“Kupitia mpango huo, kila nchi itapata nyongeza ya megawati 26.6 katika gridi zao za Taifa. Hili linatarajiwa pia kuimarisha uunganishwaji wa umeme wa kikanda baina ya nchi hizo tatu ambazo pia ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” ilisema.

Iliongeza  wakati wa utekelezaji wa mradi huo eneo la Afrika Mashariki kutakua na ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 500 wenye weledi na vibarua kutoka nchi tatu zitakazonufaika na mradi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles