20.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Mradi wa maji wa Sh. bilioni 5.6 kuhudumia wakazi 25, 500 Mkuranga

Tunu Nassor, Dar es Salaam 

Wakazi 25,500 wa Wilaya ya Mkuranga Desemba mwaka huu wanatarajiwa kupata huduma ya maji safi baada ya kukamilika mradi wa maji katika eneo hilo.

Akizungumza katika ziara ya aliyoifanya wilayani humo, leo April i11, Ofisa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema tayari uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 600 umekamilika.

Amesema kesho Aprili 12,  wataanza kazi ya ulazaji mabomba kwa umbali wa kilomita 15.

“Mkandarasi wa ujenzi wa tenki ataanza rasmi mwezi Mei na mradi utagharimu Sh Bilioni 5.6,” amesema Luhemeja.

Aidha Luhemeja amewaomba wakazi wa eneo hilo kuwa wavumilivu kwa kuwa kazi zinaendelea na zitakamilika kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles