21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

MRADI WA KUSAMBAZA GESI ASILIA MAJUMBANI WAFIKIA ASILIMIA 76

PATRICIA KIMELEMETA, Dar es Salaam


MENEJA Mradi wa usambazaji wa gesi majumbani  Dar es Saaalam, Denice Byarushengo, amesema kazi ya kusambaza mabomba ya gesi asilia kwa wananchi imekamilika kwa asilimia 76.8.

Byarushengo alisema hayo jana wakati akimueleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC), Kapuulya Musomba kuhusu hatua ambazo mradi huo umefikia.

Byarushengo alisema mradi huo unalenga kuunganisha kKwanda cha Coca Cola Kwanza Ltd. na Kiwanda cha Mafuta cha BIDCO   na wateja   takribani 1000 wa majumbani.

Alisema kazi hiyo pia imekwenda sambamba na kusimika  mtambo wa kupunguza mgandamizo ambao nao  umekamilika kwa asilimia 97.

“Uunganishaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 88.6, ulazaji na ufukiaji wa mabomba umekamilika kwa asilimia 56.9.

“Viainisho sita  vya bomba linapopita vimeshawekwa na ujenzi wa daraja  la waenda kwa miguu umekamilika kwa asilimia 90,”alisema Byarushengo .

Alisema  mradi huo utahusisha kuvuka mto Ubungo   na  barabara ya Ubungo Maziwa na ya Mandela, kazi  ambayo hadi sasa imekwisha kukamilika.

Alisema kwa   barabara ya Ubungo Maziwa kazi  imekamilika kwa asilimia 50, huku kwa barabara  ya Mandela kazi iko mbioni kuanza.

Alisema mradi huo utawezesha upatikanaji wa gesi asilia ya kutosha katika bomba linalotoka  Ubungo kwenda Mikocheni kupitia barabara ya Sam Nujoma  na kusambaza gesi kwa wateja wa majumbani katika maeneo ya Ubungo, Shekilango, Mlalakuwa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza na Mikocheni.

Musomba alieleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao utaunganisha bomba kubwa la gesi asilia la urefu wa kilomita 7.8  na lile la Ubungo kwenda Mikocheni   na uwezo wa kusafirisha  gesi ya  futi za ujazo milioni 7.5    kwa siku.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles