23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MRADI WA KINYWE LINDI WAFUZU MAZINGIRA

Na Joseph Lino

KAMPUNI ya Uchimbaji madini ya kinywe (graffiti) kutoka Australia, Walkabout Resources, imepanga kukusanya Dola za Marekani milioni 1.25 kwa ajili ya kuendeleza mradi wa kinywe wa Lindi.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, hii imefuatia baada ya kukamilika kwa utafiti yakinifu kuhusiana  na mradi huo ambao unaonyesha kuwa imara katika uchumi wa mradi huo.

Mwenyekiti wa Walkabout, Trevor Benson, alisema katika taarifa yake kwamba kipaumbele cha kampuni hiyo ni kukamilisha ufadhili mradi wa Lindi.

“Majadiliano yanayoendelea ingawa hayajakamilika, yanaendelea vizuri pamoja na kupokea maombi kutoka  Ulaya na China,” alisema.

Walkabout inatafuta njia mbalimbali za kupata ufadhili wa mradi unaoendelea na kampuni inatarajia kupitisha michakato mbalimbali ya madeni pamoja na mchanganyiko wa mikataba na thamani ya mali.

Wakati huo huo, kampuni ilibainisha kuwa imepata  cheti cha mazingira kwa ajili ya mradi ambayo ni hatua kubwa katika udhibiti na kimefungua njia kwa ajili ya kuwasilisha maombi ya leseni ya uchimbaji wa madini kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Maombi hayo yapo katika hatua za mwisho na yatawasilishwa hivi karibuni.

Mwaka jana Walkabout Resources ilitangaza kuwa ilikuwa inatarajia kuanza ujenzi katika mradi wa Kinywe Lindi mwaka huu.

Kampuni hiyo miaka michache iliyopita ilisema mradi wa Lindi unaweza kuzalisha tani 25,000 hadi 40,000 za madini ya grafiti kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 20.

Pia iliwahi kusema kuwa mradi utahitaji mtaji wa uwekezaji wa Dola za Marekani  milioni 35 hadi 40, ikiwa na gharama ya uendeshaji wa dola 290 na 350 kwa tani na kufanya mradi wa Lindi kuwa mzalishaji wa gharama ya nchini katika miongoni mwa wachimbaji.

Utafiti unaonyesha kuwa mradi huo una thamani halisi ya takribani dola milioni 169 kwa uzalishaji wa tani 25 000 kwa mwaka hadi unaweza kuongezeka kufikia dola milioni 304  katika uzalishaji wa tani 40 000 kwa mwaka.

Pia mradi wa Lindi ulikadiriwa kuwa wastani wa mzunguko wa fedha kati ya Dola milioni 24 na 43 kwa mwaka. Wakati huo uzalishaji wa mapato kabla kodi unakadiriwa kuwa kati ya dola milioni 26 na 45.

Aidha, kampuni inasema ubora wa hali ya juu ya rasilimali ya madini yaliyopo katika mradi huo unatoa ushindani katika kupunguza gharama za uendeshajii na kuwezesha uzalishaji wa madini bora ya kinywe  yenye uwezo wa kupata mauzo ya bei nzuri katika soko la ushindani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles