22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mradi usambazaji umeme ‘Peri Urban’ wazinduliwa Dodoma

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mradi mkubwa wa usambazaji umeme jijini Dodoma ‘Peri Urban’ umezinduliwa jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine utakamilisha usambazaji wa umeme katika maeneo yote yaliyokuwa yamesalia kufikiwa na nishati hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kijiji na Kata ya Chihanga, nje kidogo ya jiji la Dodoma (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Awamu ya Pili katika maeneo yaliyo pembezoni mwa jiji la Dodoma, Juni 16, 2021.

Akizindua mradi huo jana, Jumatano Juni 16, 2021, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema mradi huo umegharimu kiasi cha Sh bilioni 17.3 ambapo umelenga kusambaza umeme katika kwenye maeneo yote ya mitaa 222 ambayo hayajafikiwa jijini humo.

“Kupitia mradi huu wa umeme, mtaunganishiwa kwa Sh 27,000 kama nilivyosema awali na imani yangu ni kwamba utachochea shughuli za uchumi na kijamii hivyo niwaombe sana muitumie vizuri fursa hii ambayo Rais Mama Samia Suluhu Hassan ametutaka tutekeleze mara moja ili tuwaondolee adha wananchi kwa kukosa umeme.

“Kwa hivyo basi na mimi namuagiza Mkandarasi Cylex kutoka Sri Lanka kuanza utekelezaji mara moja ili baada ya mwezi mmoja na nusu nije niwashe mwenyewe hapa,” amesema Waziri Kalemani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amewataka wananchi wote kuhakikisha wanaitumia nishati hiyo kama kichocheo cha kujiletea maendeleo na hasa kwenye kuongeza ufaulu kwa watoto wa shule ambao watapata muda mrefu wa kujisomea katika mazingira rafiki kuliko ilivyokuwa awali.

Awali, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde aliishukuru serikali kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya usambazaji wa umeme ya Peri Urban na Densification ambayo kukamilika kwake kutaliwasha Jiji lote la Dodoma na hivyo wananchi kutumia nishati hiyo kujiletea maendeleo mbali mbali hasa katika sekta za kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles