27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Mradi nyumba za makazi Magomeni Kota mbioni kukamilika

Na KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

MRADI wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika Januari 2021. 

Akizungumza jana jijini hapa wakati akikagua maendeleo ya mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Msanifu Majengo Elias Mwakalinga alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa mradi huo ambao unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unakamilika serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni tisa ili kuumalizia.

Alisema kuwa hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 81na kwamba familia 656 zinatarajiwa kupatiwa nyumba hizo.

“Mradi ulichelewa kukamilika kwa wakati kutokana na serikali kuchelewa kutoa fedha lakini hivi sasa imeshatoa fedha zote na kwamba kwa mujibu wa TBA tunatarajia mradi utakamilika mwezi Januari na kwakuwa serikali ya sasa haitaki mchezo iwapo uzembe utafanyika utakaosababisha kushindwa kukamilika kwa mradi basi mtaona majipu yanatumbuka,” alisema Msanifu Majengo Mwakalinga.

Alisema katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, serikali imetenga fedha kwaajili ya kukarabati nyumba katika maeneo mbalimbali ya nchi ambazo serikali imezichukuwa ikiwa ni pamoja na kuzijenga zile zitakazolazimika kujengwa.

Alisema miongoni mwa nyumba zinazotarajiwa kufanyiwa ukarabati ni zile zilizopo katika maeneo ya Wazo Hili jijini Dar es Salaam.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Msanifu Majengo Daud Kondoro alisema katika kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, kazi inafanyika kazi usiku na mchana na kwamba hata vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa mradi huo vinatoka hapa hapa nchini. 

Alisema kuwa kutokana na kuwa serikali imeshawakabidhi pesa zote za kuweza kukamilisha mradi huo wanatarajia kuukamilisha ndani ya muda walioupanga.

Mradi huo utakaotumia gharama nafuu na kwa kuzingatia thamani ya fedha ikiwa ni pamoja na kuunganisha makazi na miundombinu ya huduma muhimu hadi kukamilika unatarajiwa kughalimu  shilingi bilioni 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles