27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MRADI MAGADI SODA WAHITAJI SH BILIONI MOJA

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

ZAIDI ya Sh bilioni 1.3 zinahitajika katika awamu ya utafiti wa kiuchumi na kiteknolojia katika mradi wa Kiwanda cha Magadi Soda, kilichopo Bonde la Engaruka, wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Tayari utafiti ulishaonyesha uwapo wa magadi soda katika eneo hilo, unaofikia mita bilioni 4.7 za ujazo na kila mwaka ujazo huo unajiongeza kwa mita milioni 1.9 za ujazo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi hivi karibuni wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Ramson Mwilangali, alisema wanachosubiriwa sasa ni upatikanaji wa kiasi hicho cha fedha.

Mwilangali, aliyeongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, aliyetembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools kinachomilikiwa na NDC, alisema kazi ya utafiti huo inaweza kuchukua takribani miezi sita hadi nane.

“Baada ya utafiti wa awali uliobaini ubora na wingi wa magadi yatakayozalishwa, sasa tunaingia kwenye utafiti kuangalia masuala ya kiuchumi na kiteknolojia katika mradi huu yanaweza kutekelezwa vipi,” alisema Mwilangali na kuongeza:

“Hapo tutakuwa tumekamilisha kiwango kikubwa sehemu ya mradi, tunachosubiri ni fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.3, tukizipata wakati wowote tunaweza kuanza awamu hiyo ya utafiti. Lakini pia uzalishaji ifikapo 2020 hadi 2022.”

Alisema mita bilioni 4.7 za ujazo za magadi soda zilizogundulika katika utafiti wa awali eneo la Engaruka na Selela zinaweza kutumika kwa miaka 500 ijayo.

Alisema baada ya kukamilika utafiti wa kiuchumi na teknolojia, hatua itayofuatia ni utafiti wa athari za mradi katika mazingira na jamii, utakaochukua takribani miezi minne hadi sita au zaidi, kulingana na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) litakavyoelekeza.

Pia alisema kwa sasa Halmashauri ya Monduli inaendelea na kazi ya kuthaminisha mali zilizopo katika maeneo mbalimbali ya mradi huo.

Kugunduliwa kwa kiasi hicho cha magadi soda baada ya Ziwa Natron kuingia katika mvutano wa kimazingira na kukwamisha mradi huo eneo hilo, kunaifanya Tanzania kuwa ya tatu kwa utajiri wa magadi soda, nyuma ya Uturuki na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles