Mr Blue aiisusa nyumba miaka mitano

0
2650

GLORY MLAY

MSANII wa Hip hop, Kheri Rajabu ‘Mr Blue’, nasema kuwa, aliikaa miaka mitano bila kuingia kwenye nyumba aliyemjengea mama yake mzazi kabla ya kufariki dunia.

Akizunguma na MTANZANIA jana, Mr. Blue, alisema alimjengea mama yake nyumba hiyo ili akaanze maisha mengine ya muziki Ulaya lakini ilishindikana baada ya mama yake kupata ajali ya pikipiki.

“Nyumba ilikuwa imekamilika na ndio nilienda kumkabidhi mama yangu funguo za nyumba hiyo, lakini kabla ya kuingia alipata ajali ya pikipiki akafariki, hivyo siokuingia ndani takribani mika mitano.

“Kwasababu niliona uchungu kuwa nimemjengea mama nyumba kabla hata ya kuingia alifariki, hivyo sikutamani kuiona, lakini baadae maisha yaliendelea na ndipo ninapoinshi kwa sasa,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here