24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mpogolo: Walioanza kujipitisha mapema CCM hawatateuliwa

Oscar Assenga, Korogwe

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kura za maoni za kuwachuja wagombea wa nafasi mbalimbali zitakuwa nyepesi kwa sababu kimeweka mfumo utakaowabaini  wasio na sifa ya kupeperusha bendera yake.

Kimesema kupitia mfumo huo, wanaokiuka taratibu ikiwamo kujipitisha kabla ya wakati, kutoa rushwa kutumia ukabila, udini na wabunge na madiwani walioshindwa kuwajibika kwa wapiga kura wao, watakuwa hawana nafasi ya kupitishwa.

Msimamo huo ulitolewa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rodrick Mpogolo, alipokuwa akizungumza na viongozi wa chama hicho wakiwamo wabunge na madiwani wa majimbo mawili ya Wilaya ya Korogwe.

Mpogolo ambaye pia aliitumia ziara hivyo kujitambulisha baada ya kuteuliwa na kamati kuu ya CCM kuwa mlezi wa chama Mkoa wa Tanga, alisema kupitia mfumo huo hakuna mgombea atakayeonewa kwa sababu unafuata katiba na kanuni ya chama hicho.

Alisema wale walioanza kujipitisha mapema kwenye kata na majimboni, watambue kwamba wanapoteza bure muda na raslimali zao kwa sababu kupitia mfumo huo hawatateuliwa na wengine watafukuzwa uachama.

Kuhusu wabunge na madiwani walioshindwa kutekeleza majukumu ya kuwahudumia wapiga kura wao, aliwataka watambue kuwa hawatanusurika kwenye mchujo huo.

“Tunao mfumo mzuri wa kuwapata wagombea wenye kufaa kuiletea CCM ushindi wa zaidi ya asilimia 85, itambulike kwamba haki ya kugombea ni ya kila mwanachama lakini jukumu la kumteua mwenye kufaa kupeperusha bendera yetu ni la CCM,” alisema Mpogolo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, alisema chama hicho kimejipanga kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba ikiwamo kurejesha Jimbo la Tanga na viti vya udiwani vilivyokuwa vinashikiliwa na vyama vya upinzani baadaya uchaguzi wa mwaka 2015.

Katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Mkomazi Jimbo la Korogwe vijijini kupitia Chadema, Abbas Mahuna alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles