25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

Mpinga ubaguzi na mwanasheria wa Mandela afariki dunia

JOHANNESBURG

MWANASHERIA maarufu wa haki za binadamu na ambaye amewahi kumtetea Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amefariki dunia akiwa na miaka 92.

Mwanasheria  huyo, George Bizos, aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini humo baada ya kuwatetea viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwamo Rais Mandela aiyemtetea wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi alifariki dunia juzi.

Baada ya shughuli za utetezi kuwatetea viongozi mbalimbali nchini humo Bizos alikiwa miongoni mwa waasisi wa Katiba mpya ya nchi hiyo.

Familia yake ilieleza kuwa mwanbaharakati huyo alifariki dunia nyumbani kwake kifo kilichotokana na sababu za kawaida.

Akitangaza kifo cha mwanasheria huyo Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa,  alisema kuwa mwanaharakati huyo wa haki za binadamu alitoa mchango mkubwa katika demokrasia ya taifa hilo la kusini mwa Bara la Afrika.

Rais Ramaphosa alimwelezea kuwa alikuwa ‘kichaa’ wa sheria na kwamba kifo chake huzuni kubwa kwa Taifa hilo huku taasisi ya Mandela ikidai kuwa jabali jingine katika historia ya nchi hiyo limeanguka.

Bizos alifahamika zaidi kwa kazi yake alipofanya kazi na hayati Mandela ambaye kwa mara ya kwanza walikutana walipokuwa wakisoma masomo ya sheria jijini Johannesburg kabla ya kujitokeza kumtetea yeye na wapinga ubaguzi wenzake mahakamani.

Bizos alikuwa mmoja wa mawakili waliomwakilisha Mandela katika kesi yake ya uhaini ya mwaka 1956 na ile ya Rivonia ambayo yeye na wanaharakati wengine wa kupinga ubaguzi wa rangi walihukumiwa kifungo cha maisha jela 1964 kwa walipotuhumiwa kutaka kuipindua serikali ya kibeberu ya nchini hiyo.

Bizos anasifiwa kwa kuongeza maneno “if needs be” kwenye hotuba maarufu ya hayati Mandela kwenye kesi hiyo, ambayo alisema alikuwa amejitayarisha kufa.

Bizos alizaliwa nchini Ugiriki lakini alihamia Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 13 kama mkimbizi wa Vita ya Pili ya Dunia. Kabla ya kuhamia nchini humo yeye na baba yake waliwasaidia wanajeshi saba wa New Zealand kuutoroka utawala wa kinazi ulioitwaa Ugiriki.

Alishindwa kuuendelea na masomo kwa kipindi fulani na kujikuta akifanya kazi katika duka moja la kigiriki baada ya kuwasili Johannesburg akiwa hajui kiingereza, hata hivyo baadaye alipata mafunzo ya sheria katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.

Baada ya kukomeshwa kwa utawala wa watu wachache nchini humo alisaidia kuandiaka Katika mpya ya nchi hiyo.

Pia alitapa nafasi ya kuziwakilisha familia za wapinga ubaguzi wa rangi waliouawa wakati wa harakati hizo katika tume ya ukweli na usuluhishi.

Katika moja ya kesi zake za kukumbukwa ni pale alipofanikisha familia  34 za wafanyakazi wa migodini waliouawa na polisi nchini humo kulipwa fidia na Serikali.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles