25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MPINA ATUMBUA WATATU KWA UVUVI HARAMU

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasimamisha kazi watumishi watatu kutokana na kudaiwa kujihusisha katika uvuvi haramu.

Pia amesema endapo suala la uvuvi haramu halitakoma ndani ya kipindi cha mwaka mmoja atajiuzulu.

Amewataja watumishi hao kutoka Kitengo cha Usimamizi wa Uvuvi (FRP) ambao wanatuhumiwa kuikosesha serikali mapato kuwa ni Ofisa Mfawidhi Rodrick Mahimbali, Mhasibu, Julius Magabe na Kaimu Ofisa Mfawidhi, Thomas Donkoli.

Akizungumza katika Kituo cha Uvuvi cha (TAFICO) jijini Dar es Salaam alikotembelea leo, Mpina amesema atahakikisha katika kipindi chake cha mwaka mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha uvuvi haramu unakwisha mapato serikali yanaongezeka sambamba na uwekezaji mkubwa katika sekta ya uvuvi.

Aidha, amesema yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja ama nyingine na biashara haramu ya uvuvi atafilisiwa mali zake sambamba na kupelekwa mahakamani.

“Hatuwezi kukosa mapato kupitia uharibifu unaofanywa na waroho wa fedha, hatuwezi kukosa kitoweo ni lazima suala hili lidhibitiwe iwe kwa kuwafilisi na kuwapeleka mahakamani wahusika wakuu na itakuwa fundisho kwa wengine wenye lengo la kufanya hivyo.

“Uvuvi haramu unahatarisha uwepo wa samaki na viumbe hai baharini na ni vyema kuelewa kuwa katika asilimia 100 ya samaki wanaoteketezwa katika uvuvi huo ni asilimia 10 pekee ndio wanatoka nje,” amesema Mpina.

Amesema halmashauri ambazo zitashindwa kudhibiti uvuvi huo au kuchukua hatua pia ataziondoa katika orodha ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na samaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles