27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

MPIGAPICHA MTANZANIA ANG’ARA TUZO ZA EJAT

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAMMPIGAPICHA wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Jumanne Juma, ameibuka mshindi wa tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2017.

Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, huchapisha magazeti ya MTANZANIA, Dimba, Bingwa, Rai na gazeti la Kiingereza la The African.

Juma alinyakua tuzo hiyo juzi usiku jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi akiwa amefungana na Omar Fungo wa Mwananchi.

Juma na Fungo walikabidhiwa zawadi zao kutokana na ubora wa picha zilizoingia katika mashindano huku Alexander Sanga Daily News akishika nafasi ya mshindi wa pili.

Katika tuzo hiyo mwanahabari Vivian Pyuza wa CGM ya Tabora aliibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya tisa ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2017.

Pyuza aliwashinda washindani wengine watatu katika nafasi hiyo ya juu ambao ni Salome Kitomari wa Nipashe, Tumaini Msowoya wa Mwananchi na Gerald Kitabu wa Guardian.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles