24.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MPENZI WA LAUREN ATOKA JELA

LONDON, ENGLAND


MPENZI wa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Lauren Goodger, Joey Morrisson, ameachiwa huru baada ya kutumikia jela miaka tisa.

Morrisson alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 16 kutokana na tuhuma za kumiliki silaha bila kibali maalumu, utekaji nyara pamoja na ubakaji.

Dada ya Morrisson, Charlotte, alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya kaka yake mara baada ya kutoka jela.

“Maneno yangu hayawezi kuelezea jinsi furaha niliyonayo baada ya kaka yangu kutoka jela, alikuwa ndani kwa miaka tisa na sasa yupo huru ni furaha ambayo haina mfano,” aliandika Charlotte.

Hata hivyo, Lauren alishindwa kuzuia hisia zake na kudai kuwa ana furaha kubwa kuona mpenzi wake yupo huru, pia ni kama ndoto kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles