25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

MPANGO WA KUMNG’OA JAJI MARAGA WAFICHUKA

NAIROBI, KENYA

NJAMA za kumng’oa Jaji Mkuu wa Kenya (CJ), David Maraga na Msajili Mkuu wa Mahakama (CRJ), Anne Amadi zimefichuka.

Imebainika kuwa njama hizo zinaendeshwa na wabunge wa Chama cha Jubilee, waliopanga kuwasilisha hoja bungeni dhidi ya Jaji Maraga na Amadi mara watakapofuzwa na kuzoea shughuli za kibunge.

Chama cha Mahakimu na Majaji wa Kenya (KMJA) kimesema mpango huo unahusiana na uamuzi wa Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya urais ya Agosti  8, mwaka huu.

“Mpango ni kumzushia CJ na CRJ mashtaka yasiyokuwapo kisha kupitisha azimio bungeni litakaloruhusu kuchunguzwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa (EACC), si kwa sababu ya ukweli wa tuhuma bali kuchafua taswira zao,” kimefichua chanzo kinachofahamu njama hizo.

Chanzo hicho, kilisema EACC itatumika kama ‘mkuki wa kisiasa’ kwa sababu wapangaji wa njama hizo wanaelewa kuwa hawawezi kuwaondoa CJ na CRJ kupitia Tume ya Utumishi ya Mahakama (JSC).

“Wanataka kumpakazia mashtaka ya uongo,” kilisema chanzo hicho cha kibunge.

Katibu Mkuu wa KMJA, Bryan Khaemba, alisema hawatachoka kutetea uhuru wa mahakama.

“Tunafahamu mpango wa idadi fulani ya wabunge wa kumng’oa mheshimiwa CJ na  CRJ kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais. Nataka kuwakumbusha wapanga njama hawa kuwa maana halisi ya utawala wa sheria, ni kwamba nchi inatawaliwa na sheria si watu,” alisema Khaemba.

Njama hizo zinakuja muda mfupi tu baada ya Mbunge wa Nyeri Mjini, Ngunjiri Wambugu kuwasilisha ombi CRJ akitaka kuondolowa kwa Jaji Maraga, ambaye ni mwenyekiti wa JSC wakati Amadi akiwa katibu.

Akihutubia vyombo vya habari, mbunge huyo alidai kwamba Jaji Maraga ”aliwashinikiza” wenzake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi kinara wa Jubilee, Rais Uhuru Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria Septemba Mosi, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles