23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MPANGO AJIUNGA MFUKO WA PSPF

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo, kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya afya.

Akizungumza jana baada ya kutembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba wakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea.

“Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi,” alisema Dk. Mpango.

Dk. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

“Mheshimiwa, Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda na machinga na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama,” alisema Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, wakati akimkabidhi kadi yake Waziri Mpango

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles