22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Mourinho: Mliwahi kumhukumu Pogba

Paul Pogba
Paul Pogba

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho, amesema kuwa vyombo vya habari viliwahi mno kuhukumu uwezo wa mchezaji wake, Paul Pogba, aliyejiunga na timu hiyo akitokea timu ya Juventus ya Italia.

Mourinho alitoa kauli hiyo baada ya mchezaji huyo kuifungia timu yake ya Manchester United mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya  Fenerbahce, katika mchezo wa Ligi ya Europa  uliochezwa juzi Uwanja wa  Old Trafford.

Lakini Mourinho  alisema wachambuzi walikuwa na haraka ya kuhukumu uwezo wa mchezaji huyo kabla ya kumpa muda wa kuonesha kipaji chake.

“Baadhi ya watu walikuwa wakizungumza maneno mabaya kuhusu Pogba ndani ya saa 48 tu alizofika Old Trafford.

“Siwezi kuwataja majina, ndiyo maana nimezitaja media, tunajua Pogba ni mchezaji mzuri, anahitaji muda wa kuonesha ubora wake,” alisema Mourinho.

Mourinho alisema anaufahamu mchezo wa soka ipasavyo na kuongeza kuwa timu za Ligi Kuu England zinacheza tofauti na ligi nyingine.

“Kila kitu katika ligi hii ni tofauti, hivyo Pogba anahitaji muda wa kujipanga zaidi, kwani anajiamini, licha ya kusemwa sana kwamba ni mchezaji mbaya na hafai kucheza Manchester United,” alisema Mourinho.

Pogba alikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza kikosi cha kwanza katika mchezo uliopita dhidi ya Liverpool.

Hata hivyo, Mourinho alisema angependa kumtumia winga Jesse Lingard, Juan Mata na Anthonio Martial, lakini hajui mfumo ambao atatumia ili kuwachezesha wote kwa pamoja.

“Mimi si mbaya, lakini sijafahamu  mbinu na mfumo utakaowezesha kuwatumia winga wanne kwa pamoja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles