29.3 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Mourinho kung’oa mtu Roma, Barca kumekucha, Arsenal…

Roma, Italia

KITENDO cha Jose Mourinho kuajiriwa na Roma kinamaanisha kiungo anayetakiwa na Liverpool, Lorenzo Pellegrini, ataondoka klabuni hapo.

Ni kwa sababu Mourinho atamsajili kiungo aliyefanya naye kazi Manchester United, Nemanja Matic.
CHANZO: Mirror

Barca, Aguero kumekucha!
NI rasmi sasa Barcelona wameanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Sergio Aguero.

Aguero ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu na atatimka akiwa mchezaji huru.
CHANZO: Sky Sports

Arsenal kinara kumfukuzia Bissouma

KLABU ya Arsenal iko mstari wa mbele katika mbio za kumfukuzia kiungo wa Brighton, Yves Bissouma.
Hata hivyo, bado Tottenham, West Ham na Everton nazo zinaendelea kuitolea macho huduma ya mchezaji huyo.
CHANZO: Express

Silva kuipasua United bil. 112/-

MANCHESTER United italazimika kutumia Pauni milioni 35 (zaidi ya Sh bil. 112 za Tanzania) kuinasa saini ya straika wa Eintracht Frankfurt, Andre Silva.

Taarifa hiyo ni ya mabosi wa Frankfurt wakisema hawaoni tatizo la kumwachia Mreno huyo mwishoni mwa msimu huu.
CHANZO: Express

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,631FollowersFollow
542,000SubscribersSubscribe

Latest Articles