23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mourinho anabebwa na takwimu za timu, Guardiola ana tabia zake binafsi?

jose-mourinhoMANCHESTER, England

KATIKA miaka ya hivi karibuni, upinzani kati ya makocha Jose Mourinho na Pep Guardiola umeibuka kuwa kivutio kwenye ulimwengu wa soka.

Kinachovuta hisia za mashabiki wengi wa kandanda ni pale makocha hao wanapokutana na jinsi ambavyo wamekuwa wakitupiana  maneno makali hata kabla ya timu zao kuingia uwanjani.

Kwa mara ya kwanza leo wawili hao watakutana wakiwa Ligi Kuu ya England.

Mourinho akiwa na Manchester United, Guardiola atakuwa na mahasimu wao, Manchester City, katika mchezo mkali wa ‘Manchester derby,’ utakaochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Kabla ya mchezo wa leo utakaochezwa saa 8:30 mchana, Guardiola na Mourinho wamekutana mara 16.

Katika mitanange hiyo, Guardiola ndiye anayeonekana mbabe mbele ya hasimu wake huyo, ambapo ameibuka na ushindi mara nane.

Moja kati ya mechi hizo, Guardiola aliibuka na ushindi wa penalti.

Mourinho ameshinda mechi tatu, huku zilizobaki tukizishuhudia zikitoka sare.

Ukiachana na upinzani mkali wa makocha hao, timu wanazozinoa sasa, yaani Man United na Man City nazo ni hasimu.

Rekodi inaonesha kuwa kwa mara ya mwisho timu hizo za jijini Manchester zilikutana Machi 20, mwaka jana.

Katika mtanange huo wa kuwania Taji la Ligi Kuu England, vijana wa Old Trafford waliibuka kidedea baada ya kuwabanjua wapinzani wao bao 1-0.

Hiyo ilikuwa ni Manchester derby ya 171 katika historia ya Soka la England.

Historia inaonesha kuwa katika michezo hiyo, Man United imeibuka na ushindi mara 71, huku wenzao wa Etihad wakishinda mara 49.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles