31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Mourinho agoma kumuuza Rooney

wayne-rooneyMANCHESTER UNITED, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho, amesema huenda akamuondoa nahodha wa timu hiyo katika kikosi cha kwanza lakini si kumuuza kwa klabu nyingine.

Rooney ambaye leo anatimiza miaka 31, hakuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichoibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi ya Europa dhidi ya Fenerbahce.

Hata hivyo, nyota huyo ameondolewa kucheza kikosi cha kwanza katika michezo mitatu iliyopita ya Ligi Kuu England.

Hali hiyo inadaiwa inatokana na kuporomoka  kwa kiwango cha nyota huyo ambaye anadaiwa kutakiwa na timu ya  Shanghai SIPG inayoshiriki Ligi Kuu ya China ‘Super League’.

Mourinho alisema kamwe hatathubutu kufanya uamuzi wa kumuuza nyota huyo  aliyejiunga na timu hiyo tangu mwaka 2004 akitokea timu ya Everton.

“Hapana, kamwe sitofanya uamuzi huo kwa aina ya mchezaji kama Rooney, kwani ni  mchezaji  mwenye historia kubwa katika klabu hii, binafsi sitofanya kosa kama ambavyo makocha wengine wangefanya kwake.

“Nilimweka benchi katika michezo mitatu kutokana na kiwango chake kushuka, ingawa ilikuwa vigumu kufanya hivyo kwake na kwangu,  kutokana na historia yake.

“Ni vigumu kumweka mchezaji mkongwe benchi ukizingatia idadi ya michezo aliyocheza katika timu ya taifa na klabu yake,” alisema Mourinho.

Mourinho alisema soka ni shughuli ambayo wengine wanaiongoza katika uamuzi sahihi na ambao si sahihi, lakini mtazamo wake kwa nyota huyo ni sahihi.

Kocha huyo anaamini kwamba baada ya nyota huyo kubadilishwa nafasi yake  uwanjani  na  kocha wa zamani wa timu hiyo, Louis van Gaal na timu ya taifa ya England, Roy Hodgson,  kumechangia kuporomoka kwa  kiwango chake.

“Nafikiri suala hili linazua maswali mengi sana kuhusu nafasi yake uwanjani na maisha yake ya baadaye, pia kwa wachezaji ambao hawajawa na uwezo wa kujiamini uwanjani wanaotakiwa kulielewa vizuri jambo hili.

“Haiwezekani  kumchezesha  namba sita hadi  nane  au  tisa, kumi hadi namba sita, Rooney kwangu mimi ni mchezaji mshambuliaji,” alisema Mourinho.

Mourinho alisema kwa kipindi chake atakachoifundisha timu hiyo, nyota huyo hataweza kucheza namba sita au kiungo uwanjani, bali atacheza kama mshambuliaji wa pili uwanjani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles