23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 24, 2021

MOTO WAZUA TAHARUKI AICC

WAJUMBE wa Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF unaondelea mchana huu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha, wamelazimika kusitisha mkutano huo baada ya kuzuka kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme.

Hitilafu hiyo inadaiwa kusababishwa na moja ya taa katika ukumbi wa Simba AICC kupiga shoti na kusababisha mfumo mzima wa umeme kukorofisha.               

Hali hiyo imesababisha wajumbe hao kusitisha mkutano wao ili kupisha mafundi kurekebisha hitilafu hiyo ambapo walifanikiwa kutengeneza.

Hata hivyo, moto huo haukusababisha madhara yoyote ya kibinadamu na tayari tatizo hilo limerekebishwa ambapo wajumbe wamerejea kuendelea na mkutano huo.     

 

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,967FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles