31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mos Def aomba kuwa raia wa Afrika Kusini

Mos DefWESTERN CAPE, AFRIKA KUSINI

NYOTA wa muziki wa hip hop raia wa Marekani, Dante Smith ‘Mos Def’, anayekabiliwa na mashtaka ya uhamiaji nchini Afrika Kusini bila kufuata sheria ameomba apewe uraia wa nchi hiyo.

Msanii huyo alikamatwa na familia yake wakati akijaribu kuondoka nchini humo kurudi nchini Marekani huku akiwa na kitambulisho cha kusafiria kisicho chake.

Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa Machi mwaka huu, huku msanii huyo akiiomba mahakama ya Western Cape jana kwamba yeye pamoja na familia yake waruhusiwe kubaki nchini humo kwa kupewa uraia.

Hata hivyo, mahakama bado haijaeleza lolote juu ya ombi la msanii huyo, ila wanatarajia kuweka wazi baada ya hukumu yake inayotarajiwa kutolewa Machi mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles