26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Morrison ataka Yanga iheshimiwe

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison amesema kuwa, chochote atanachokifanya akiwa na Simba, Yanga itahusika kwa sababu ndio timu iliyomleta katika soka la Tanzania.

Morrison alijiunga na  Yanga Januari mwaka huu kwa mkataba wa miezi sita uliofikia tamati Julai 15, kisha kutimkia Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Licha ya kuitumikia Simba kwa muda mfupi, kiungo huyo amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.

Nyota huyo raia wa Ghana, ameichezea Simba michezo mitatu ikiwemo miwili ya kirafiki na mmoja wa Ngao ya Jamii kuashiriki funguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili hii.

Alianza kuichezea Simba mchezo wa kirafiki wa kimaraifa dhidi ya Vital’O, uliopigwa siku ya kilele cha tamasha la klabu hiyo ‘Simba day’.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 6-0, huku Morrison akifunga bao moja.

Alipangwa kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, huku yeye akifunga bao moja na kuchagia jingine na mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC ambao Simba ilishinda mabao 6-0, kwenye uwanja huo.

Lakini kabla ya kuidhinishwa kukipiga Simba, Morrison aliingia kwenye mgogoro na Yanga ambayo inadai kuwa ina mkataba naye mwingine wa miaka miwili ulioanza kufanya kazi baada ya ule wa awali kumalizika.

Mgogoro huo ulimfanya Morrison kupeleka shauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),ambalo kupitia kamati yake ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilimtangaza kuwa huru  baada ya kubaini kasoro kwenye mkataba wa Yanga na mchezaji huyo uliowasilishwa kwake.

Akizungumza maisha yake mapya ya kisoka akiwa na Simba, Morrison alisema licha ya sintofahamu iliyojitokeza kati yake na waajiri wake wa zamani, bado ataendelea kuwaheshimu viongozi wa Yanga na watu wote waliohusika kumleta Tanzania.

“Huenda Simba wasingemjua mtu anayeitwa Morrison kama sio Yanga, lazima Yanga ipewe heshima yake kwa sababu bila wao nisikuwa nacheza mpira Tanzania, kwangu bado ni watu muhimu katika maisha yangu ya soka.

“Sina ugomvi na yoyote kutoka Yanga yaliyotokea ni sehemu ya changamoto za maisha, nitawaheshimu nikiamini mafanikio nitakayoyatapa ndani ya  Simba yametokana na wao kunileta Tanzania na wengine kuweza kuniona,”alisema Morrison.


Akizungumzia maisha yake ndani ya Simba, Morrison alisema anayafurahia kwa sababu atapata changamoto mpya ambazo zinamuongezea kujituma uwanjani.

“Nimekutana na changamoto mpya zinazoniongezea kujituma uwanjani, nawaahidi mashabiki wa Simba, nitaendelea kufanya kile ambacho wanatamani kukipata kutoka kwangu,  lengo likiwa kuisaidia timu iendelee kupata mataji.”  

Sssssssssssssssss

Kaduguda aiondoa Simba Bongo

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

BAADA ya msimu uliopita kutwaa mataji matatu katika mashindano manne iliyoshiriki katika ardhi ya Tanzania,Wekundu wa Msimbazi Simba wamepania kusaka mafanikio zaidi kimataifa.

Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mwina Kaduguda,alipozungumza na MTANZANIA  hivi karibuni.

Kaduguda maarufu Simba wa Yuda alisema kiu yao kwa sasa ni kufika fainali ya  Ligi ya Mabingwa Afrika, michuanoa mbayo kikosi chao kitashiriki msimu ujao.

“Mataji ya mashindano ya ndani tuna asilimia 100 yakuchukua bila kikwazo chochote,mipango iliyopo ni kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kama tukishindwa sana tuishie fainali.

“Simba ina kikosi kipana na cha ushindani kimataifa, tuna kila sababu ya kufika tunapopataka hasa ukizingatia aina ya wachezaji tulionano kuna timu gani hapa Tanzania ya kushindana na Simba, bila shaka hakuna na haitakuwepo kwa miaka mitatu ijayo,”alisema Kaduguda.


Kaduguda alisema, kulingana na kikosi cha sasa cha Wekundu hao, timu zinazoweza kuipa changamoto ni zile vigogo za Afrika.

“Levo(hatua)ya Simba ni timu kama Al Ahly na sio hizo ndogo za hapa Tanzania, hii ina maana kuwa, bado tuna miaka mitatu mingine ya kutawala katika soka la hapa nyumbani.”   

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa Simba, , Sven Vandenbroeck , alisema Ngao ya Jamii waliyoinyakua wikiendi iliyopita, ni ishara kuwa msimu wa 2020/21 utakuwa na mafaniko kwao.

“Tumeanza vizuri Ligi Kuu kwa kuchukua Ngano ya Jamii tukiwa na ushindi wa kuanzia mabao mawili, hii ni ishara nzuri kuelekea safari ya kuchukua mataji yote ambayo Simba tutashiriki kwenye mashindano yake,”alisema kocha huyo.

Mataji matatu iliyotwaa Simba ndani ya mwaka huu ni Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho maarufu Kombe la Azam na Ngao ya Jamii, huku ikichemsha kwenye Kombe la Mapinduzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles