32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

MORRISON AILIZA SIMBA MBELE YA JPM

MOHAMED KASARA – DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI  wa kimataifa wa Ghana, Benard Morrison, ameifungia Yanga bao pekee lililoipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jana Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo uliorindima kuanzia saa 11 jioni, ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyeushuhudia akiwa sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika(Caf), Ahmad Ahmad. 

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 50, lakini ikisalia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, baada ya kushuka dimbani mara 25, ikishinda michezo 13, sare nane na kupoteza mchezo mmoja, ikiiacha Azam, katika nafasi ya pili na pointi zake 51, huku Simba licha ya kupoteza mchezo wa jana iliendelea kukamata uongozi ikiwa na pointu 65.

Ikumbukwe kuwa, timu hizo zilipoumana, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Januari 4, mwaka huu, dakika tisini zilimalizika kwa sare ya mabao 2-2. 

Dakika ya 11, mkwaju wa Ditram Nchimbi ulitoka nje ya lango la Simba, baada ya kupokea pasi ya Mapinduzi Balama.

Dakika ya 22, Kocha wa Simba Sven Vandenbloeck alilazimika kumtoa  beki Erasto Nyoni baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Kenedy Juma.

Dakika ya 26, Kiungo Jonas  Mkude, alilimwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi, Benard Morrison.

Dakika ya 29, kipa wa Yanga, Metacha Mnata alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya Luis Miquissone na Clatous Chama.

Dakika ya 39, beki Shomari Kapombe wa Simba alilimwa kadi ya njano, baada ya kumfanyia madhambi Morrison.

Dakika ya 40, Papy Tshishimbi alilimwa kadi ya njano, baada ya kumfanyia madhambi Kapombe.

Dakika ya 43, Morrison aliifungia Yanga bao la kuongoza kwa mkwaju wa adhabu ndogo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa madhambi na Mkude.

Dakika ya 45, beki wa Yanga , Juma Abdul alilimwa kadi ya njano, baada ya kumfanyia madhambi  Mohamed Hussein.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika kwa Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza, kiligawanyika vipindi viwili, Yanga ikianza kuuteka mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Simba, kabla ya Wekundu kuamka na kujibu mara kadhaa ingawa hawakuweza kupata bao.

Dakika ya 55, Kocha wa Yanga, Luc Eymael alifanya mabadiliko alimtoa, Morrison baada ya kuumia na nafasi yake Patrick Sibomana kabla ya Simba kutoka Kahata na kuingia Deo Kanda.

Dakika ya 62, kipa wa Simba, Aishi Manula alifanya kazi ya ziada kupangua mkwaju wa Nchimbi.

Dakika ya 69, Sven alimtoa Kagere na kumwingiza Hassan Dilunga kabla ya Eymael kumtoa Mapinduzi Balama na kuingia Deus Kaseke.

Dakika ya 88, Menata alipangua kiki ya Chama aliyepokea pande la Dilunga.

Dakika ya 89, Eymael alimtoa Feisal Salum na kumwingiza Kelvin Yondan, mkakati ulioonekana una lengo la kulinda bao lao.

Dakika ya tisini, Keseke angeweza kuiandikia Yanga bao la pili baada ya mkwaju wake kugonga mwamba.

Dakika 90 za mwamuzi Martin Sanya kutoka Morogoro zilikamilika kwa Yanga kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Mengine yaliyojiri

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles