28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

MOROCCO ATANGAZA NGORONGORO HEROES MPYA

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23,  (Ngorongoro Heroes), Hemed Morocco, jana alitangaza  kikosi cha wachezaji 38 watakaoingia kambini Novemba 6 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Burundi.

Ngorongoro Heroes wanatarajia kucheza na Burundi Novemba 14 na watarudiana  baada ya wiki Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika mwakani nchini Misri.

Morocco atasaidiwa na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar na Bakari Shime wa JKT Tanzania.

Wachezaji waliotangazwa jana ni Metacha Mnata,  Ramadhani Kabwili, Godfrey Paul, Godfrey Paul, Abdallah Shaibu, Ally Salim, Abutwalib Mshed,  Kibwana Shomari, Ayoub Mohamed, Keneth Godfrey.

Wengine ni Amos Abel, Dickson Kibabage, Mohamed Abdallah, Hance Masoud, Ally Ally, Bakery Nondo,  Dickson Job, Ally Msengi, Ibrahim Hamad,  Awadhi Salum,  Cleofas Anthony,  Baraka Gamba,  Adolf Mtasingwa, Vitalis Mayanga,  Hussein Seleman  na Kelvin Nashon.

Wengine ni Mustafa Muhsin, Salum Kihimbwa, Ismail Aidan, Geofrey Mwashiuya, Issah Abushesh, Cliff Antony,  Hassan Salum, Athanas Mdamu, Kelvin Sabato.

Adam Salamba, Eliud Ambokile, Mbaraka Yussuph, Habib Kiyombo na Super Julio.

Akizungumza Dar es Salaam jana kocha mkuu wa kikosi hicho, Morocco, alisema timu hiyo itaingia kambini Novemba 6 mwaka huu katika Hosteli ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Tumepata kikosi cha wachezaji 38 kwa mechi mbili tutakazocheza na Burundi ambayo tutaanza ugenini na kurudiana nyumbani Novemba 20 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles