27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Morgan Heritage waanza kusaka vipaji Afrika

CHRISTOPHER MSEKENA


KUNDI nyota la muziki nchini Jamaica, Morgan Heritage, limeanza kutekeleza mradi wake wa kusaka vipaji vya muziki barani Afrika kwa kumsaini msanii wa Nigeria, Fayross kwenye lebo yao, CTBC Music Group.


Akizungumzia ujio wa fursa hiyo msemaji wa Morgan Heritage, Mojo alisema lebo ya CTBC Music Group imeungana na Sony Music katika kusambaza muziki kidijitali ulimwenguni kote hivyo wasanii wa Afrika ikiwamo Tanzania wataanza kunufaika.


“Tutafanya kazi na wasanii wanaochupikia kwenye sekta ya burudani kwa aina zote za muziki. Hii ina maana kuwa wasanii Watanzania watafikiwa na kupata dili kubwa kama hizi.


“Wimbo mpya wa msanii wetu mpya, Fayross tumepanga utoke Novemba 6, mwaka huu na utaweza kununuliwa na watu wote duniani,” alisema Mojo.
Aliongeza kwa kuwataja wasanii kutoka Tanzania kama Foby, Ruby, Wini, Nash Mc, J Zebra na Lau wa John kuwa wanaweza kufikiriwa kusainiwa na lebo hiyo ya Morgan Heritage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles