23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

MORATA AWAPASHA MASHABIKI UCHWARA

MDRID, HISPANIA


MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Alvaro Morata, amewatolea uvivu mashabiki wasiokuwa na uvumilivu na wanaokata tamaa mapema pale mchezaji anapofanya vibaya kwa kueleza ukweli kuwa wachezaji si mashine kuna wakati wanachoka.

Morata alieleza hayo Jumatano iliyopita wakati timu yake ilipoifunga Bayern Munich mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, Ujerumani.

Mhispania huyo wakati anaitumikia timu ya Juventus ya Italia, aliwahi kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid akiwa mbele ya mashabiki 78,000 na baadaye mbele ya mashabiki 70,000 katika mchezo wa fainali dhidi ya Barcelona.

Aidha, Morata aliwahi kucheza dhidi ya Atletico Madrid mbele ya watu 61,000 jijini Lisbon, Ureno na timu ya PSG katika Uwanja wa Stade de France, jijini Paris mbele ya mashabiki 76,000.

Hata hivyo, Morata anasema licha ya kucheza mbele ya mashabiki wote hao aliogopa zaidi alipokutana na mashabiki 1,000 katika ukumbi wa muziki wa Teatro Calderon jijini Madrid, ingawa usiku huo kila mmoja alionekana kumuunga mkono.

Wakati ‘show’ ikiendelea ikiongozwa na DJ Antonio Diaz au kwa jina la utani ‘El Mago Pop’ Morota aliitwa kucheza katika jukwaa na mpenzi wake Alice Campello.

Morata alijiunga na Juventus akitokea Madrid kwa euro milioni 20 wakati huo akiwa na umri wa miaka 20.

Katika msimu huo, Morata aliweza kutwaa mataji mawili; lile la Ligi Kuu Hispania na Ligi Kuu Italia, huku Juventus ikifika fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini katika msimu wake wa pili alihaha kurejea katika kiwango chake baada ya kupita siku 100 bila kufunga bao huku akijaribu kila namna kwa kubadili hadi mitindo ya nywele na aina ya gari, hata hivyo mambo hayakuwa mazuri kwake.

“Watu hufikiri wachezaji ni mashine, hawafikiri kwamba kufanya vibaya muda mwingine kunasababishwa na matatizo binafsi pamoja na familia.

“Nilikuwa nakaribia kupotea kabisa katika ulimwengu wa soka, si kwa sababu nilishindwa kufunga bao ila nilikuwa katika ugomvi na watu ambao ni muhimu kwangu,” anasema Morata.

Morata anasema aliondoka kwao akiwa bado kijana mdogo kwenda kucheza Juventus huku Real Madrid wakimwambia watamrudisha nyumbani japo maamuzi ya mwisho yatakuwa ni yake.

“Wakati huo sikufahamu hatima yangu ni ipi, kila kitu nilichofanya kiliniathiri sana nikaruhusu kuathirika hadi uwezo wangu ndani ya uwanja,” anasema Morata.

Morata anasema msimu wa pili ulikuwa ni mgumu kwake hakuweza hata kumiliki mpira katika miguu yake na alipoulizwa kuhusu hali hiyo alijibu: “Hali hii inanitokea na huzuni nilionao baada ya kuondoka nyumbani, lakini kipa Gigi Buffon, alikuwa pamoja na mimi, kuna wakati aliniambia kama nahitaji kulia niende kufanya hivyo nyumbani.

“Nilikuwa na bahati baada ya kukutana na Alice ambaye baadaye alikuja kuwa mpenzi wangu na maisha yangu yalibadilika, natarajia kufunga naye ndoa siku chache zijazo,” anasema Morata.

Hata hivyo, Buffon anadhani kuwa Morata ana kila kitu kinachohitajika kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani kutokana na ubora wake ndani ya uwanja.

“Katika nafasi yangu jambo la msingi ni kufunga bao, mbali na kuwa katika matatizo mashabiki hawaelewi sababu zinazofanya mshambuliaji kushindwa kufanya vizuri uwanjani.

“Mashabiki wanashindwa kuelewa kuna wakati maisha yanaweza kubadilika muda wowote na ukashindwa kufanya vizuri,” anasema Morata.

Nyota huyo anasema wakati anafikiria kurudi katika timu yake ya sasa nchini Hispania, alipigiwa simu nyingi kutoka England.

“Makocha wengi kutoka England walinipigia na kunieleza kuwa wanataka nijiunge katika timu zao hata hivyo nilikubaliana nao kwa kuwa nilikuwa na hamu ya kucheza England.

“Wakati huo sikufahamu nini Madrid walikuwa wanafikiri kuhusu mimi kwa kuwa nilitambua Juventus walitakiwa kunirejesha hivyo sikutambua kama jambo hilo lingefanikiwa,” anasema Morata.

Morata anasema kuna wakati alizungumza na kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino na kocha wa Chelsea, Antonio Conte, hata hivyo mipango ya uhamisho ilikwama baada ya Madrid kurejesha Hispania.

“Madrid walisema hawataki kuniuza kokote lakini wakati huo Chelsea walikuwa wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 60 ili kunisajili lakini ilishindikana.

“Baba yangu alisema kati ya timu hizo mbili moja itanyakuwa ubingwa England na kweli alikuwa sahihi kwani kuna kila dalili Chelsea kufanya hivyo,” anasema Morata.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles