24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Morata,  Alcacer pasua kichwa  Hispania

untitled-2-recovered-recovered-recovered-recovered

Martin Mazugwa na Mitandao,

MOJA kati ya nchi zilizojaliwa kuwa na vipaji murua vya soka, huwezi kuacha kuwataja mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, timu ya Taifa ya Hispania ‘La roja’.

Timu hiyo iliyosheheni nyota wengi wenye vipaji vya kusakata  soka  katika sehem mbalimbali uwanjani, ambao  wanaocheza sehemu mbalimbali barani Ulaya.

Kuna vita  mpya imeanza kuibuka ya kuwania namba  katika kikosi cha Hispania kati ya nyota wawili wenye uwezo mkubwa wa kuchana nyavu, Paco Alcacer  anayekipiga FC Barcelona na Alvaro Morata mchana nyavu wa matajiri wa jiji la Madrid, Real Madrid.

Alcacer mmoja kati ya washambuliaji wenye uchu na mabao,  aliwahi kucheza katika kikosi cha vijana cha  Valencia  kwa misimu minne akizifumania nyavu mara 42 katika michezo 64 .

Kwa upande wa kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya La liga, mchana nyavu huyo ameshuka dimbani mara 92 na kufumania nyavu mara 30 uwezo ambao si wa kubeza.

Nyota huyo aliyepitia katika ngazi ya vijana ya timu ya Taifa ya nchi hiyo akicheza jumla ya michezo 41 na kupasia nyavu mara 29, ameitwa katika kikosi cha wakubwa cha Hispania mara 13 na kufunga mabao sita.

Alcacer  mwenye umri wa miaka 23 ameenda kuongeza nguvu katika pacha iliyofanya vizuri msimu uliopita iliyokuwa inaundwa na Messi, Suarez na Neymar yaani MSN.

Catalunya wamefanya usajili huo kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji, pindi nyota wake wa kikosi cha kwanza wanapokuwa na majeruhi.

Kwa upande wake Alvaro Morata, yeye amerudi nyumbani kwa mara nyingine baada ya  kuondoka Santiago Bernabeu msimu wa mwaka 2014 na kujiunga na miamba ya Serie A, alikodumu kwa misimu miwili akicheza jumla ya michezo 63 na kufunga mabao 15 .

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 asiyependa masikhara anapokuwa karibu na lango, ameanza kuuwasha moto katika mechi mbili alizocheza kwa kupachika bao moja.

Morata aliyetesa misimu miwili akiwa na miamba ya Italia na mabingwa wa Serie A , Juventus ‘Kibibi kizee cha Turin’ alikoonyesha uwezo wa hali ya juu.

Mtajiri hao walimuuza nyota huyo alipokuwa kinda, mara baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya jijini Madrid.

Nyota huyo alikulia katika kikosi cha vijana wa Real Madrid akicheza michezo 83 na kufunga mabao 45, uwezo uliosababishwa apandishwe kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ambapo alicheza jumla ya michezo 37 na kuingia nyavuni mara kumi.

Mshambuliaji huyo pia amecheza katika kikosi cha timu ya vijana ya Hispania michezo 21 na kuifungia mabao 16 uwezo ambao haufai kubezwa hata kidogo, nyota huyo aliitwa katika kikosi cha timu ya Taifa mara ya mwisho 2014 amecheza jumla ya michezo 15 na kuifungia mabao nane.

Morata amerudi na kujiunga na pacha hiyo ambayo aliikimbia misimu miwili iliyopita, amerejea tena kuipa nguvu pacha hiyo yenye uchu wa mabao inayoundwa na, Bale na Benzema Cristiano yaani BBC.

Wawili hawa wanampa wakati mgumu kocha mkuu wa La roja, kuwa nani anafaa kujumuishwa katika kikosi chake kikosi kitakachoanza  maandalizi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia nchini Urusi 2018.

 

Kocha mkuu wa kikosi hicho, ni mmoja kati ya walimu wenye heshima na walioandika rekodi katika nchi ya Hispania, Vicente del Bosque, anatarajia kufanya maamuzi magumu  ya kumchagua mchezaji yupi atafaa katika kikosi chake.

Kitendo cha nyota hao kujiunga na timu kubwa, itakuwa presha kwa kocha huyo iwapo hatomjuisha mmoja kati yao ukizingatia kikosi cha hivi sasa kina washambuliaji wengi wenye umri mkubwa.

Del Bosque ili kazi ya kwenda Urusi iwe nyepesi hana budi kupata straika wa uhakika, ambaye ataweza kuamua matokeo katika mechi ngumu .

 

Tayari mwalimu huyo anaye mshambuliaji  mkorofi wa klabu ya Chelsea Diego Costa, ambaye naye amekuwa hafanyi vizuri siku za karibuni licha ya mechi iliyopita kukifungia kikosi hicho mabao mawili katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 nchi Urusi.

 

Costa ambaye amekuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha La roja, huku straika mkongwe Fernando Torres anayekipiga Atletico akianzia nje, wachezaji hawa wawili wote uwezo wao umekuwa wa kawaida.

 

Del Bosque hana jinsi ni lazima aongeze mmoja kati ya nyota hawa wawili, ambao siku za karibuni wameonekana kuimarika huku wakiwa na uchu wa kufanya vizuri kila kukicha.

 

Ni muda muafaka kwa kocha huyo mkongwe kuanza kuwaamini vijana hao, ambao wote wapo chini ya makocha bora kwa hivi sasa Morata ambaye yupo chini ya Zinedine zidane na Alcacer yupo chini ya Luis Henrique.

 

Del Bosque aliwaacha wachezaji hao katika mashindano ya Euro yaliyofanyika nchini Ufaransa, huku kikosi chake kikiambulia patupu katika mashindano hayo yaliyomalizika kwa Ureno kuibuka mabingwa.

 

Kikosi cha La roja kina washambuliaji wengi na wenye uwezo mkubwa Barani Ulaya, wanaofanya vizuri lakini  uwepo wa washambuliaji hao wawili kutoka klabu hasimu nchini Hispania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles