30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Morales asema yeye bado ni rais Bolvia, amwangukia Papa

LA PAZ, BOLVIA

ALIYEKUWA rais wa Bolivia, Evo Morales ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa au Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis kusuhulisha mzozo wa kisiasa uliomlazimisha kujiuzulu na kukimbilia uhamishoni nchini Mexico.

Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press mjini Mexico City, Morales amesema anaamini kuwa yeye bado ni rais wa Bolivia kwa sababu Bunge halijaridhia barua yake ya kujiuzulu.

Wakati wa mahojiano hayo Morales amesisitiza pia nia yake ya kurejea nchini Bolivia kutoka uhamishoni nchini Mexico.

Hayo yanajiri wakati rais wa mpito wa Bolivia, Jeanine Anez amefuta uwezekano wa Morales kugombea urais katika uchaguzi unaokuja.

Anez amesema Morales hawezi kushiriki katika uchaguzi mwingine kwa sababu katiba ya Bolivia inazuia rais kuongoza zaidi ya mihula miwili mfululizo.

Anez ameyasema hayo wakati maelfu ya waandamanaji wakimiminika katika barabara za mji mkuu La Paz kumuunga mkono msoshalisti huyo aliyejiuzulu na kumpinga kaimu kiongozi huyo mpya.

Waandamanaji wanadai kuwa kung’atuka kwa Morales hakukuwa hatua ya kujiuzulu bali ni matokeo ya mapinduzi na hivyo wanamtaka arejee nyumbani.

Serikali ya mpito imetangaza juzi kuwa mazungumzo na chama cha Morales cha Movement for Socialism – MAS yameanza katika jaribio la kuleta amani katika nchi hiyo iliyogawika vikali.

Rais wa mpito Anez, mwenye umri wa miaka 52 amesema Morales hawezi kushiriki katika uchaguzi mwingine wowote mpya kwa sababu katiba ya Bolivia inamzuia rais kuongoza kwa mihula miwili mfululizo.

Kwa hiyo chama cha MAS kinahitajika kumtafuta mgombea mwingine.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles