28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

MONGELLA KUMFUATILIA MTOTO ALIYEBAKWA NA MTENDAJI

jOHN mONGELLA

Na JUDITH NYANGE- MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema Serikali itahakikisha inafuatilia matibabu na masomo ya mtoto mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyabulugoya, aliyebakwa na Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, James Chilagwire (42).

Sambamba na hilo, Mongella amesema atahakikisha anafuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili haki itendeke.

Kauli hiyo aliitoa juzi alipoitembelea familia hiyo ili kufahamu maendeleo ya mtoto huyo aliyefanyiwa unyama huo Novemba 16, mwaka jana saa 1:00 jioni katika Mtaa wa Nyabulugoya.

Inadaiwa Chilangwire alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumkuta akiwa ndani peke yake na kumbaka.

Baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alifikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure na kufanyiwa uchunguzi na madaktari ambao walibaini kuwa ameharibiwa vibaya sehemu za siri na kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambako alifanyiwa upasuaji.

Mongella akiwa hapo alisema amepata taarifa kuwa mama wa mtoto huyo wanapokea vitisho kutoka kwa watu hivyo alimtaka kutotishika kwa lolote huku akimwagiza Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyaguluboya kulisimamia suala hilo hatua kwa hatua.

“Tumesikia unapokea vitisho sana kutoka kwa watu mbalimbali, niseme tu usitishike kwa lolote, Serikali itahakikisha mtoto wako anapona na kurejea shuleni pamoja na kufuatilia mwenendo mzima wa kesi yako mpaka pale hukumu itakapotolewa na mahakama,” alisema Mongella.

Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo, Ester Otieno, alisema mtoto wake kwa sasa bado ana maumivu sehemu za siri na hajapona kutokana na upasuaji aliofanyiwa hivyo ameshindwa kuhudhuria shuleni kuendelea na masomo yake.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyaguluboya, Keffa Dickson, alimshukuru Mongella kwa kumtembelea mama huyo kwani ilifikia kipindi walikata tamaa.

Alisema mama wa mtoto huyo ni mjane ambaye anaishi katika mazingira magumu na pia anategemewa na watoto wengine wanne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles