25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MONGELLA AWATAKA WAISLAMU KUENDELEA KUFANYA IBADA

Na CLARA MATIMO

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema kama   walivyotenda wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya ibada na kuliombea taifa amani.

Alitoa wito huo kwa waislamu hivi karibuni   katika baraza la Idd EL Fitr kwenye  msikiti wa Shia.

Alisema bila amani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana  katika taifa lolote  duniani hivyo ni vema waendelee kudumisha upendo, kuheshimiana na kufanya ibada.

“Mungu anasikia maombi ya waja wake mnapokutana wawili ama watatu kwa ajili ya jina lake naye anakuwa katikati yenu , hivyo nawasihi maombi mliokuwa mkiyafanya kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan  myaendeleze  taifa letu lizidi kuwa na amani.

“Ombeni bila kuchoka iwe kwa Waislamu au Wakristo wote tuungane kuliombea taifa letu amani   Mungu azidi kutusaidia amani tuliyonayo idumu,”alisema Mongella.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, aliwataka Waislamu waendelee kumtumikia Mungu na kufanya kazi zilizo halali kwa bidii  wajiingizie kipato kitakachowawezesha kukidhi mahitaji yao na familia zao.

“Nawasihi ndugu zangu Waislamu msifungulie kila kitu endelezeni matendo mema mliyokuwa mkiyatenda kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Mungu atawabariki.

“Hatutegemei kuona muislamu ambaye amefunga mwezi mzima wa Ramadhan halafu baada ya kumaliza mfungo akakamatwa kwa    kuvunja sheria,”alisema Tesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles