31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MONGELA AMTAKA RMO KUKABILIANA NA EBOLA

Na JUDITH NYANGE


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Leonard Subi, kutoa muongozo wa jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa   anapotokea mgojwa.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoa tahadhari   kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa huo.

Hiyo ni  baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO)    kutangaza kulipuka kwa ugonjwa huo    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika jimbo la mpakani na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tahadhari hiyo ilitolewa  hasa katika mikoa ambayo inayopakana na DRC na mikoa iliyotakiwa tahadhari hiyo ni Mwanza, Kagera Kigoma, Katavi na Rukwa na Songwe.

Mongella alikuwa akizungumza juzi  wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

Alisema ni vema muongozo huo ukatolewa mapema ili anapotokea mgonjwa anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo taarifa zipatikane mapema na asiweze kuambukiza watu wengi.

“Mikoa iliyotajwa ambayo inaweza kuwa rahisi kupata ugonjwa wa ebola  ni pamoja na Mwanza.

“Naomba  utolewe mwongozo katika maeneo yote ya kuingia na kutoka Mkoa wa Mwanza pamoja  na  usafirishaji   watu waweze kutambua na kama kuna dalili zozote za ugonjwa huo  taarifa zitolewe mapema  tusije tukachelewa ,” alisema Mongella.

Vilevile aliitaka bodi hiyo kuisimamia hospitali hiyo na kuhakikisha inaongeza mapato yake kutoka Sh bilioni moja zinazokusanywa sasa kwa mwaka hadi angalau Sh bilioni 2.5 au 3 kwa mwaka na kuhakikisha wanatumia mifumo ya eletroniki  kudhibiti ubadhirifu.

“Tumeongeza makusanyo yetu kutoka Sh mlioni 500 hadi kufikia Sh bilioni 1 kwa mwaka.

“Lakini kwa idadi yetu ya watu tulipaswa kufikia Sh bilioni 2.5 hadi 3 kwa mwaka, bodi hii isimame  imara kuhakikisha malengo hayo ya makusanyo yanafikiwa.

“Kuna tabia ya wizi wa dawa na vifaa vingine vya kutolea  huduma na hili hakikisheni linakomeshwa.

“Haiwezekani kila siku watu wapewe maelekezo, gari linalotoka na kiasi kadhaa cha dawa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) lakini zinazofikishwa katika kituo husika si zote, niwatake watumishi wa afya waache ubadhilifu na wizi na kuwa waadilifu,” alisema Mongella.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi, alisema mahitaji halisi ya watumishi wa idara afya katika mkoa huo ni watumishi 7,582.

Alisema  watumishi waliokuwapo kabla ya   uhakiki walikuwa  watumishi 3,552 ambao asilimia 48 ya mahitaji yote ya watumishi.

Dk. Subi alisema katika kukabiliana na tishio la mlipuko wa   ebola wiki ijayo itaanza kutolewa  elimu kwa wadau wote wa  afya Mkoa wa Mwanza  kuhusu ugonjwa huo.

Alisema pia itawekwa   mikakati ya pamoja ya namna ya kuudhibiti  na tahadhari za kuchukua endapo utatokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles