26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Monalisa: Tuandae filamu zinazohamasisha ‘sickle cell’

monalisaELLY MHAGAMA (TUDARCO) NA GRACE KASONDE (SJMC)

MWIGIZAJI wa filamu nchini, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ ameomba wasanii wenzake wawe na utamaduni wa kuandaa filamu zitakazohamasisha Watanzania kuhusu ugonjwa wa upungufu wa damu (sickle cell).

Monalisa alitoa hamasa hiyo jana, katika uzinduzi wa bonanza kuhusu ugonjwa huo lililofanyika Upanga, jijini Dar es Salaam.

“Mimi binafsi nitakuwa balozi wa kuelimisha wasanii wenzangu kuhusu ugonjwa huo na pia naweza kufanya filamu ya hamasa kuhusu ugonjwa huo, hivyo wasanii tuwe mabalozi, pia wazazi tusiwafiche watoto wetu, tuwapeleke wakapimwe kwa kuwa ugonjwa huu unamaliza watoto walio chini ya miaka mitano,” alisema Monalisa.

Mmoja wa wenye ugonjwa huo, Khadija Abdallah, alisema ugonjwa huo unahitaji matunzo ya karibu kwa kuwa haueleweki muda gani unabadilika, hivyo ameomba wasinyanyapaliwe.

Nao wachezaji wa Simba SC, Musa Hassan Mgosi na kocha msaidizi wa timu hiyo, Selemani Matola, walisema watakuwa mabalozi bora na pia watazungumza pamoja ili wajue wanachangiaje kampeni hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles