30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Monalisa ataja siri za urembo wake

Na Glory Mlay

MSANII mkongwe wa filamu, Yvonne Cherrie ‘Monalisa’, ametaja sababu zinazomfanya aendelee kuwa na mvuto.

Mrembo huyo amedai sababu kubwa ni kutotumia mafuta ya kuchubua mwili kama wanavyofanya wengine.

Amedai katika maisha yake hakuwahi kushawishiwa na mtu ambaye amejichubua na ndio maana hakutaka kuingia huko.

“Watu wengi au wasanii wengi wanaona kujichubua ndio fasheni hawajui kuwa wanapoteza muonekano wao na kuwa watu waajabu, wanazeeka mapema unaweza kukutana na mtu mdogo kuliko mimi lakini ngozi yake haitamaniki kwa sababu ya mkorogo,” alisema.

Aliongeza kwa kusema, wanatakiwa kujitambua na kutunza ngozi yao, wanaokimbilia weupe hauna faida na mwisho wa siku  ngozi inaungua na kupoteza muonekano wake wa kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles