MOI YAPATA MKURUGENZI MPYA

0
473

Na MWANDISHI WETU​, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemteua Dk. Respicious Lwezimula, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI).

Nafasi hiyo ilikuwa inakaimiwa na Dk. Othman Kiloloma.

Dk. Lwezimula anachukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi tangu mwaka 2014  baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI kustaafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja uteuzi huo ulianza jana.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Lwezimula alikuwa Daktari Bingwa MOI.

“Nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI ilikuwa wazi tangu mwaka 2014 kutokana na yule aliyekuwepo kustaafu,” ilisema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here