28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Moi yaingiza mitambo ya upasua ubongo bila kufungua fuvu

Aveline Kitomary -Dar es salaam

TAASISI ya Tiba ya Mifupa (MOI) imeingiza nchini mitambo ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) itakayokuwa msaada mkubwa katika tiba hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi, mitambo hiyo imewasili bandari ya Dar es salaam na inatarajiwa kusimikwa siku chache katika taasisi hiyo.

Ujio wa mitambo hiyo mipya na ya kisasa inayotoka Nchini Ujerumani, ni juhudi za Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya hapa nchini.

” Mitambo, Vifaa vingine pamoja na ukarabati wa Chumba vimegharamiwa na Serikali  kwa gharama ya Sh bilioni 7.9.” Alieleza Patrick Mvungi.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Radiolojia,  Dk. Mechric Mango alisema huduma hiyo itaweza kupunguza rufaa za nje ya nchi.

“Maabara hiyo itakuwa na faida ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi, hapo awali wagonjwa walikuwa wanahitaji upimaji wa mishipa ya damu ya kichwani hawa wote walikuwa wanapelekwa nje ya nchi kwahiyo mashine itakapofungwa hawataenda nje na itaokoa fedha nyingi,” alisema.

Dk. Mango alisema uhitaji wa mashine hizo ni mkubwa kutokana na kutoa vipimo na matibabu kwa wakati mmoja.

“Uhitaji wa huduma hiyo  ni mkubwa sana hapa tuna ‘deal’ na kichwa, uti wa Mgongo na mifupa  sasa wale ambao wana matatizo kwenye ubongo moja wapo ya vipimo vinavyohitajika vikubwa ni hivi.

“Wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kufanya au mishipa ya damu ambayo sio ya kawaida  hao wanahitaji hiki kipimo pia mashine hii inatumika kutoa matibabu kuna wale wenye uvimbe kwenye ubongo pia tutatumia hii mashine kwa wale wenye mishipa ya damu kwenye uvimbe ili kuzuia damu nyingi isimwagike,”alieleza Dk. Mango.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles