31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Moi yafanyia upasuaji watoto 197

upasuajiNA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM

ZAIDI ya watoto 197 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya GSM na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI).

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana,  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,  Dk. Othman Kiloloma, alisema watoto waliofanyiwa upasuaji ni awamu ya pili ya kampeni ya kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa inayofadhiliwa na GSM na tayari wameshafanyia upasuaji watoto kwa mikoa tisa.

Dk. Kiloloma pia alisema waliweza kuwafanyia vipimo watoto 800 wenye matatizo mbalimbali, wakiwamo wa vichwa vikubwa.

“Hata hivyo, taasisi yetu inatarajia kufanya tena upasuaji wa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa awamu ya tatu na tunatarajia kutembelea mikoa mitano,” alisema Dk. Kiloloma.

Alisema mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi kama atawahishwa hospitalini mapema na kuonwa na madaktari, upo uwezekano mkubwa wa kuokoa maisha yake.

Ni vema kwa wazazi wenye watoto walio na vichwa vikubwa na mgogo wazi kuhakikisha wanawafikisha hospitali mapema watoto hao kuweza kufanyiwa uchunguzi, alisema.

Alisema mpaka sasa katika taasisi hiyo wapo watoto 60 waliolazwa kwa matatizo mbalimbali, wakiwamo waliopata ajali.

Aliipongeza Kampuni ya GSM kwa msaada wake wa kugharamia upasuaji huo kwa watoto na kuzitaka kampuni nyingine kuiga mfano huo.

Naye Ofisa Habari wa Kampuni ya GSM, Halfani Kiwambwa, alisema mbali na kufadhili upasuaji wa watoto, wameguswa na kuamua kutoa msaada  wa pampas 50,000 kwa taasisi hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia jamii nzima.

“Hii ni sehemu ya msaada ambao tunatoa kwa jamii mbalimbali kuwawezesha wananchi katika huduma za jamii,” alisema Kiwambwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles