25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

MOI YAFANYA UPASUAJI UCHAKAVU WA MISHIPA YA FAHAMU

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

MWANAMKE  mwenye umri wa miaka 45 amefanyiwa upasuaji wa kisasa wa matundu (Minimal Invasive Spine Surgery).

Upasuaji huo ulikuwa ni  kutibu tatizo lililokuwa linamsumbua la uchakavu wa misuli na mishipa ya fahamu  inayozunguka uti wa mgongo.

Upasuaji huo ulifanywa jana na madaktari bingwa wa ubongo, mgongo na uti wa mgongo wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mgongo, Ubongo na Uti wa Mgongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya BLK ya i India.

Akizungumza na waandishi wa habari, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mgongo na Ubongo wa MOI, Dk. Joseph Kahamba alisema ulifanyika na kukamilika kwa zaidi ya saa mbili.

“Tumeufanya jopo la madaktari wanne, huyo mgonjwa kwenye uti wake wa mgongo mishipa yake ya fahamu  ilikuwa imebanwa kutokana na uchakavu wa misuli na mishipa mingine inayopita kwenye uti wa mgongo na kwenye mishipa mingine ya mfumo wa fahamu,” alisema.

Dk. Kahamba alisema tatizo hilo kitaalamu linaitwa The generative spinalcanal stenosis with instability, na hutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ongezeko la uzito wa mwili.

“Kadiri mtu anavyoongezeka umri anakuwa kwenye uwezekano wa kupata ugonjwa huu lakini pia mfumo mbovu wa maisha hasa kutokufanya mazoezi na kula usiofaa husababisha uzito wa mwili kuongezeka.

“Uzito wa mwili unapoongezeka husababisha maumivu ya mgongo kuanzia eneo la shingo ambayo hushuka hadi miguuni na kusababisha ganzi kwenye miguu hali ambayo hupelekea mtu kuchoka haraka na kushindwa kutembea umbali mrefu,” alisema.

Naye Dk. Puneet Girdhan wa BLK alisema kwa kutumia upasuaji huo wamefungua tundu dogo na hivyo mgonjwa hakuhitaji kuongezewa damu.

Inaemdelea………….. Jipatie nakala ya gazeti #MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles