26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

MOI yaanzisha huduma sita mpya za kibingwa ndani ya miaka minne

Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI), Dk. Respicious Boniface amesema taasisi hiyo imeanzisha huduma sita mpya za kibingwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Novemba 22 amesema taasisi hiyo inajivunia katika uongozi huo kutokana na huduma zenye ubora kuongezeka.

“Huduma hizo mpya ni upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu (athroscopy) tayari wagonjwa 800 wameshafanyiwa huduma za upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebral aneurysm) wagonjwa watano wameshafanyiwa.

“Upasuaji wa kunyoosha vibiongo kwa watoto 12 tayari, upasuaji uti wa mgongo kupitia tundu dogo wagonjwa 120 wamepata huduma hii kuna uanzishwaji wa wodi maalumu ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo wagonjwa 355 wamefanyiwa na huduma ya dawa za usingizi pasipo kulala hii tumefanya kwa wagonjwa 250,” amesema Dk. Boniface.

Amesema huduma hii mpya imeweza kupunguza rufaa za wagonjwa nje ya nchi ambapo kwa sasa asilimia 95 ya magonjwa ya Neurosurgeries yanafanyika hapa na upasuaji wa mifupa unafanyika kwa asilimia 98.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles