25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Mohammed Enterprises yasheherekea Valentine na dereva bodaboda

Beatrice Kaiza – Dar es Salaam

kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imesherehekea siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s day’ na madereva wa bodaboda wa jiji la Dar es salaam kwa lengo la kuonesha upendo na kutoa elimu juu ya utumiaji wa vyombo hivyo.

Akizungumza na madereva hao Kamanda Mkuu wa Usalama Barabarani wa kijitonyama, Hezron Mkana amesema maendeleo ya usafiri kwa sasa yamekuwa kutokana na teknolojia na kuwa na vyombo bora kama pikipiki aina ya boxer ambavyo watu wengi wanapenda kuitumia.

“Usafiri siku za nyuma ulikuwa duni sana ila kutokana na kukua kwa teknolojia tumepata usafiri bora na hivi sasa ajali za barabarani zinaweza kuepukika kama madereva wataongoza kuonyesha umakini wakiwa barabarani,”  amesema Mkana.

Aidha amewasisitizia madereva hao kuwa wasafi wanapokua kazini kwao na kutokiuka sheria zilizowekwa na Serikali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles