MOBETTO KUZINDUA ‘LIPSTICK’ UINGEREZA

0
768


NA JESSCA NANGAWE

MWANAMITINDO Hamisa Mobetto anatarajia kuzindua rangi yake ya mdomo ‘lipstick’ nchini Uingereza Mei 5, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Milton Keynes.

Mrembo huyo, ambaye alianza kuonyesha bidhaa hiyo kipindi cha nyuma, alisema kwa sasa kila kitu kinakwenda vyema na wapo kwenye maandalizi ya mwisho ya uzinduzi huo.

“Nashukuru Mungu tumefikia pazuri na hadi sasa kila kitu kipo vizuri, nategemea mwanzoni mwa Mei tutafanya uzinduzi wetu nchini Uingereza, kabla ya kuanza kuziuza sehemu mbalimbali,” alisema Hamisa.

Katika uzinduzi huo, msanii Lulu Diva anatarajia kupamba shughuli hiyo, huku Hamisa akiwataka Watanzania wanaoishi nchini humo kumsapoti.

Hamisa anaungana na Wema Sepetu na Flaviana Matata, ambao walitumia ustaa wao kuuza urembo wa wanawake kama rangi za mdomo na kucha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here