Na JOHANES RESPICHIUS
MSANII nyota wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’, amesema hawezi kusahau alivyolikimbia jukwaa la Fiesta jijini Mwanza mwaka 2014 baada ya kupagawa na umati mkubwa wa mashabiki waliojitokeza kupata burudani.
Staa huyo wa Singo ya Adoado ameliambia Juma3tata kuwa siku hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kutumbuiza kwenye jukwaa kubwa kama hilo kitu kilichosababisha achungulie na kukimbia nyuma ya jukwaa.
“Nakumbuka kwenye Fiesta ya mwaka 2014 mkoani Mwanza nilijikuta nikilikimbia jukwaa kutokana na umati mkubwa wa mashabiki waliokuwepo kwenye uwanja wa CCM Kirumba, ile nachungulia nilikutana na watu zaidi ya elfu 20, nilishtuka nikambia nyuma ya jukwaa, baada ya kuzoea mazingira nikarudi tena jukwaani kufanya shoo,” alisema Mo Music.