23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mo Dewji: Mageuzi ya Magufuli yamechangia kuendelea kuwekeza nchini

Anna Potinus – Dar es Salaam

Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), amempongeza Rais John Magufuli kwa jitihada anazozifanya katika uongozi wake amabapo amesema kuwa mageuzi makubwa yaliyofanywa katika kipindi cha awamu ya tano ndiyo yaliyopelekea kuendelea kuwekeza nchini.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda chake cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Magufuli amekizindua.

“Mheshimiwa Rais tunaamini kwamba wale wasiokuelewa leo watakuelewa baadae na wasioelewa lengo wataeleweshwa na matokeo ambayo tunaamini hayako mbali sana kwani mageuzi makubwa chini ya uongozi wako ndiyo yaliyotushawishi kuendelea kuwekeza nchini kama unavyoshuhudia leo hii,” amesema.

“Binafsi ninashuhudia kuimarika nidhamu kwa watumishi wa umma, mkazo mkubwa serikalini, kutekelezwa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo, kupungua kwa rushwa na kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi nchini pia tumeguswa na namna ulivyoshugulikia matatizo ya wafanyabishara,” amesema.

Aidha amesema kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa na vya kisasa kinachojihusisha na uzalishaji wa unga wa ngano na wa mahindi nchini, na kwamba kampuni ilianza uwekezaji 2005 na ilianza na kiwanda chenye uwezo mdogo wa kusaga tani 240 kwa siku pamoja na uwezo wa kuhifadhi tani 20 tu za nafaka.

“Hivi sasa kiwanda kimeboreshwa kwa kuwekeza kwenye mitambo mikubwa iliyogharimu jumla ya Sh. bilioni 105 na inatumia teknolojia ya kisasa zaidi, uwekezaji huu umefanyika chini ya awamu ya tano, leo tunashuhudia kiwanda cha mahindi chenye uwezo wa kusaga tani 300 kwa siku, kiwanda cha ngano chenye uwezo wa kusaga tani 1240 kwa siku, mitambo yenye uwezo wa kupokea tani 600 kwa saa za nafaka na uwezo wa kuhifadhi nafaka hadi tani elfu 50,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles