25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

MO AIBUA ARI MPYA SIMBA

NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM


WAKATI timu ya Simba ikishuka dimbani leo kuivaa Stand United, kuachiwa huru kutoka katika mikono ya watekaji kwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, kumeibua ari mpya katika kambi ya timu hiyo ambayo leo itashuka dimbani kuumana na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mo alitekwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyoko Oysterbay Bay, jijini Dar es Salaam, alikoenda kwa ajili ya mazoezi ya mwili ‘gym’, kisha watekaji wakatokomea naye kusikojulikana, kabla ya kupatikana usiku wa kuamkia jana, eneo la Gymkhana, jijini Dar es Salaam, baada ya kutelekezwa na watekaji.

Hadi anapatikana, tajiri huyo namba 17 Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes, tayari alikuwa amekaa katika mikono ya watekaji kwa siku tisa.

Kupatikana kwake kulikuja saa kadhaa baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro, kuwaonyesha waandishi wa habari picha ya gari aina ya Toyota Surf alilodai lilitumika wakati wa utekaji wa mfanyabiashara huyo.

Mbali ya kuonyesha picha hiyo, Sirro alisema walifanikiwa kubaini dereva wa gari hilo na kudai lilitoka nchi jirani ambayo hata hivyo hakuitaja na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles