26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mnyika, Mchange wavutana sakata la mauaji

John Mnyika
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUHUMA za mauaji ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa, zimeendelea baada ya Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Chadema, John Mnyika na kada wa chama hicho, Habib Mchange kuvutana hadharani.

Hiyo ni siku chache baada ya Mchange kutoa tuhuma dhidi ya viongozi wa juu wa Chadema wakiwamo Dk. Willibrod Slaa, Freeman Mbowe (mwenyekiti wa chama), Tundu Lissu (mwanasheria) na Mnyika akidai kuwa wanasuka mipango ya mauaji dhidi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Wakizungumza jana katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV, Mchange alizidi kudai kuwa viongozi hao wanasuka mauaji dhidi ya wananchi na akamtaka Mnyika awaombe radhi Watanzania.

“Ninashangazwa Mnyika anashindwa kusema ukweli, kwani tukiwa katika uchaguzi mdogo Igunga alikuja na kuhangaika usiku kucha ili kufukia tindikali iliyomdhuru kada wa CCM, Mussa Tesha kwamba ndani ya Chadema, Slaa, Mbowe na Lissu eti hawatakiwi kuguswa.

“Huu ni uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu ya Chadema ambayo ilibariki mipango mbalimbali ya mauaji, yakiwamo ya Chacha Wangwe na hata matukio ya Morogoro, Iringa na Arusha,” alidai Mchange.

Mchange alitoa matamshi hayo mazito mbele ya Mnyika kuhusu madai yake kwamba viongozi waandamizi wa chama hicho ndiyo mabingwa wa matukio ya ugaidi na utoaji roho za wenzao.

Hata hivyo, mtangazaji wa kipindi hicho alipomhoji Mchange kwa nini madai hayo hakuyapeleka polisi kipindi chote hadi sasa ndiyo anaibuka nayo, kada huyo alisema amefanya hivyo kwa kuchukuliwa maelezo yake polisi na akawataka Mnyika na Mbowe nao wafanye hivyo.

Mchange ambaye ni mwanachama wa Chadema kutoka Wilaya ya Temeke aliwahi kugombea ubunge katika Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani mwaka 2015 na kushindwa.

Alisema viongozi wa Chadema pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wamekuwa wakitekeleza mambo hayo hasa wanapotofautiana katika msimamo na mitazamo ndani au nje ya chama.

“Dunia nzima inajua watu hawa wameshiriki kwa ukamilifu kumuondoa duniani aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Wangwe. Hii haina ubishi kwamba Mbowe, Slaa na Mnyika walijaribu mara kadhaa kutaka kumuua kwa sumu na kushindwa mpaka walipoweza kumuua kwa ajali ya kutengeneza Julai 28 mwaka 2008 wakimtumia kijana ambaye dunia nzima inamjua,” alidai Mchange.

Wakati kada huyo akirusha makombora hayo, muda wote Mnyika alikuwa mtulivu huku akionyesha a kutabasamu.

Mchange katika kipindi hicho cha Star Tv, alimshangaa Mnyika kukiri kwamba anamfahamu Mallya wakati awali alimkana kutomfahamu kwa namna yoyote.

Mchange alidai baada ya Wangwe kufariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Pandambili, Dodoma Julai 28, 2008 usiku Mnyika alizungumza na waandishi wa habari kesho yake na kumkana Deus Mallya akisema Chadema haimtambui.

“Maana yake ni nini? Ni kwamba Mnyika na Chadema walimkana Mallya kimkakati ili kukiondoa chama kwenye ushahidi wa mauaji ya kiongozi wake mkuu msaidizi,” alidai Mchange na kuhoji, “kwa nini Mnyika alimkana Mallya aliyekuwa si tu rafiki yake lakini mshirika wake mkuu kwenye harakati za ujenzi wa chama?”

Alidai baada tu ya tukio hilo, Dk. Slaa alimuagiza Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi aidhinishe malipo na vijana waliohusika wakapelekwa Mwanza na kuhifadhiwa kwenye Hoteli ya Magnum kwa zaidi ya mwaka mmoja, wakiendeshwa na dereva mmoja maarufu wa Chadema ambaye hakumtaja.

Mnyika ajibu mapigo

Akijibu tuhuma hizo, Mnyika alisema madai ya Mchange hayana ukweli ila anachofanya ni kutafuta huruma ya siasa mbele ya Watanzania.

“Suala la madai ya Igunga ya kuhusika kwangu na tindikali, mimi sikuwapo nchini nilikuwa Zambia kama mwangalizi katika uchaguzi mkuu… sasa nahusikaje.

“Ni muda mrefu chama chetu kimekuwa kikihusishwa na madai haya lakini tuliandika barua kwa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete ili aunde tume ya mahakama kuchunguza madai haya ya muda mrefu dhidi ya chama chetu mpaka sasa yupo kimya.

“Mchange anatumiwa na CCM na chama chake cha ACT ili avuruge. Iweje leo hii aje na hoja ya Wangwe au kwa kuwa ni marehemu, si jambo jema kuzungumzia suala la marehemu…nachotaka kusema ni kwamba watawala lazima wajue hawawezi kutusingizia tuhuma za mauaji wakati mikakati hii inafanywa na wao wenyewe,” alisema Mnyika.

Wiki iliyopita madiwani wawili wa Chadema waliokuwa CCM Mkoa wa Shinyanga, waliibua tuhuma hizo wakidai walitumwa waitungue helikopta ‘ iliyokuwa imewabeba viongozi wa chama hicho akiwamo Dk. Slaa.

Diwani wa Kata ya Ngokolo, Sebastian Mzuka na Zakaria Mfuko wa Kata ya Masekelo, walidai kula njama za kumuua Dk. Slaa, zikipangwa na kile walichodai mtandao mpana wa CCM na Serikali yake.

- Advertisement -

Related Articles

10 COMMENTS

  1. mmm!! amakweli hizi siasa nizamajitaka huyu kijana anayeitwa mchage nadhani anahitaji maombezi, anaonekana sio mkweli hata kidogo. kwa akili ya kawaida tu inaonekana amekosa dira na uelekeo katika siasa yeye anadhani anajijenga kumbe anajimaliza alikuwa wapi tangia wakati ule kumbe sio mtu mzuri inaonekana kitendo chake cha kuondolewa chamani ndicho kinamuuma sana CHADEMA kuweni makini na mapandikizi haya!!

    kwanini wakati wote hakuyasema haya? leo ni mwaka wa ngapi tangu afariki marehemu chacha wangwe anaonekana hana data anadai mnyika alikuwepo igunga wakati wakati huo hakuwepo inchini huoni hapo tu inaonyesha kauli zake hazina mashiko kabisaa. haya sasa ona wasaliti wenzake wanavyoubuka sasa madiwani waliosaliti wameona huko CCM sio unatakiwa uwe makini sasa wanataka kurudi hilo pia ni tatizo ukweli utabaki kuwa ukweli hakuna mtanzania mpumbavu tena utakayekuwa unamwambia mambo hayo akakuelewa watanzania kwa sasa wamekomaaa sana, ningependa kumkumbusha kuwa kila kitu huwa kinakuwa na ushahidi sasa inaonekana ushahidi wako ni mwepesi mmno! kajipange tena unaposema uongo jitahidi uwe na kumbukumbu kwani kwa sasa watanzania wanaakili sana wanajua zipi pumba na zipi ni mchele. naungana moja kwa moja na Kinyana mnyika anaonekana ukweli amekomaaa kisiasa kwamba huyu mchage anatafuta huruma ya kisiasa hana lolote.

    • Mchange wakati wa ajali ya Chacha Wange alikuwa kidato cha 6 na siasa kajiunga akiwa form I sasa aliwezaje tumika ktk hayo yote,Jenga hoja utoke kisiasa cyo vinginevyo ndugu yangu umeacha hadi chuo kwa sababu ya siasa unapoteza mwelekeo unaanza tugumu wenzio

  2. ni kweli kaka yangu machange umepoteza Dira, Kaa chini muombe mungu akusaidie usiwe unatapatapa kiasi icho, Watanzania wa sasa wanajielewa ivo kuwa na data zilizo na huhakika, acha uongo kaka iyo njia unayoingilia sio jaribu kuangalia upande wa kilimo uenda ukakutoa.siasa bado uwezi

  3. Tatizo la wanasiasa uchwara kama ndugu Mchange ni kuamini kuwa siasa ni uongo na propaganda. Hali hii ni kutokana na kuamini kuwa kila mtu anaweza kuwa mwanasiasa, imani hii siyo kweli. Mwalimu Nyerere wakati wa uongozi wake alianzisha chuo cha siasa Kivukoni kwa malengo ili kuondokana na wanasiasa uchwara wasiojua matatizo yanayowasibu wananchi. Leo hii mtu akimaliza kishahada chake ambacho kinatokana na mitihani ya kuchagua na kuandika ‘kweli’ au ‘si kweli’ basi anajiona kuwa anafaa kuwa mwanasiasa, hii ni hatari maana mpaka sasa nchi yetu inaugua ugonjwa wa kuwa na wanasiasa wasio na uwezo wa kuchambua mambo. Pole ndugu Mnyika kwa kukutana na nyang’au wa kisiasa.

  4. Binafsi nimekuja kuelewa kuwa anachokifanya Mchange ni kuganga njaa kwa hali yeyote ile iwe ni kwa gharama ya damu au la.

    Serikali ya Tanzania sio changa sana katika mambo ya kiintelijensia na wala haiwezi kupumbazwa na njaa za watu tena wenye nia mbaya ya kuchonganisha watanzania.

    Huyu bwana ikiwa alikuwa na ushahidi mkubwa wa kiasi hiki na kama kweli ni mtanzania mwenye nia njema na nchi yake na kwa hali ya kawaida na ninavyomwelewa yeye ni mtanzania anaye fahamu wazi kuwa jeshi la polisi limeweka utaratibu mzuri wa kwamba mtu akitoa taarifa sio lazima atoe ushahidi mahakamani sasa hata hilo la kuripoti polisi kwa siri nalo alishindwa na kama ndio amekumbuka kutoa sasa ushahidi huo ni baada ya muda gani na labda kitu gani kimemsukuma sasa!

    kufanya hivyo na sio wakati ule nini kilimzuia kwenda hata kwa mkuu wa polisi nchini kama labda alikuwa hawaamini polisi wote na kuwaamini kulikomjia sasa kumetoka wapi au ujasiri huo amepata wapi hawezi kutudanganya kuwa alikuwa anawaogopa akina Silaa na wenzake anapaswa kuwa mwaminifu na kumwogopa Mwenyezi Mungu hilo analifahamu wala sio jambo la kumkumsha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria hilo kwake ni geni?

    Au labda ni mtu wa kusahausahau na kama ndivyo pia hawezi kuaminika kabisa katika jamii sana sana kwa waliomtuma ndio watagundua kuwa walifikiri ni mtu makini kumbe ni bure tu ni mtu hatari sana anataka kuona damu inamwagika akifikiri yeye atakuwa salama uchonganishi anaoufanya ni mbaya sana na atambue hata aliowatuhumu wakiamua kumshitaki na kudai fidia ya kuwachafua kwa jamii hana cha kuwalipa ni masikini njaa isimfanye akapoteza utu na kutaka kuwachanganya watanzania mpuuzeeni.

    Mtu ambaye anakuja kukumbuka kuokoa majivu badala ya kuzima moto kabla haujatetekeza mbugu yote. kueleza sasa katika majukwa ya siasa anaka watanzania wamweleweje siasa za sasa ni vyama vingi tupingane kwa hoja na aepuke sana kuwa na lafiki wa kudumu kwenye siasa wala tena asiweke uadui wa kudumu pia katika nyanja za siasa hayo ni mawaidha kwake na wengine wenye kuwa na mawazo kama ya kwake.

    Nchi hii ikivurugika hakuna atayekuwa salama tena tizama tunataka kuivuruga kwa ajiri ya kuganga njaa tu ni hatari sana tafari acha kabisa jambo unalolifanya halina tofauti na kujaribu kutoboa ngarawa wakati sote tunaitegema. amani ni kitu bora kuliko kitu kingine chochote chini ya jua hili wala hili hupashwi kufundishwa na Proffersor, tulia siasa zinataka ueledi wa hali ya juu na sio kama unavyoenenda.

  5. Mambo ya kutuhumu yanayoendelea TZ, ni kamchezo fulani!
    Tuhuma nzito ya MAUAJI kama anaifahamu badala ya kuripoti kwenye vyombo vya DOLA, anaenda kuyatolea kwenye vyombo vya HABARI!!!!!!!!!!!
    Mtu wa namna hiyo anatia shaka na anaelekea anatumwa na chama tawala akichafue chama cha cdm. Hata ninyi wapelelezi jiepusheni na SIASA kwani hali hiyo itasababisha vurugu nchini kama mtawaachia ccm wafanye wanavyotaka, ninyi ni zaidi ya ccm,hakuna atakayekubali kuwakamata Viongozi wao kwa kusingiziwa halafu anyamaze tu.Nawasihi kuweni makini sana

  6. Mtu mwenye Njaa kali kama Mchange ni HATARI SANA. Tunapaswa kumuogopa huyu kijana kama UKOMA. Asipokuwa makini akaacha UPUUZI HUU ANAOFANYA SASA anajiingiza katika maisha ya kuwa na maadui wengi kwa sababu tu ya NJAA zake.

    Inasikitisha sana

  7. Watanzania ivi sasa wanauelewa mkubwa haijalishi kwamba manaelimu au lah!.huyu kijana ameonyesha udhaifu mkumbwa Mungu anasaidia hawa watu kuondoka ndani ya vyama makini kama chama cha chadema ambacho kinafanana kama wingu katika nchi yenye ukame,watu wakilitazama wanakuwa natumaini kwamba siku moja tutapata mvua .Mungu ibariki chadema.VIJANA kama mcahange
    ni tatizo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles