Na FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM
CHAMA cha Damokrasia na Maendeleo(Chadema), kimewaagiza wabunge wake kote nchini kuhoji iwapo kutakuwa na mswaada wa mabadiliko ya tume huru ya uchaguzi, ili Watanzania waweze kupata viongozi wanaowataka kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, muda mfupi kabla ya kufanya kikao na wanachama wa chama hicho Jimbo la Kibamba, alisema kuwa kuna haja ya kufanyika mabadiliko ya tume ya uchaguzi ili kuepuka machafuko kama alivyoonya juzi Rais Dk. John Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.
Kauli ya Mnyika imekuja ikiwa ni siku moja tu imepita tangu, Rais Dk. Magufuli alipowataka Wazanzibar kutorudia makosa yaliyojitokeza miaka ya nyuma, wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Mnyika alisema kuwa ni lazima kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi ambayo itaenda sambamba na kuwapo kwa haki ya kupingwa kwa matokeo mahakamani pamoja na mgombea anayekuwa peke yake kupigiwa kura ya ndiyo na hapana.
“Ni muhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi, na kesho(leo) vikao vya Kamati za Bunge vinaanza, na Bunge rasmi Januri 28, kama tunavyofahamu kwamba tayari Rais Dk. Magufuli ameshasema kwamba hataki kuona yaliyotokeo Zanzibar yajirudie basi Watanzania wote, taasisi za dini ziombee hili, Asasi za kiraia ziwaunganishe Watanzania, na vyama vya Siasa vipiganie upatikani wa tume huru ya uchaguzi.
“Na niwaombe wabunge wa Chadema kuwa mstari wa mbele katika hili wahakikishe kuwa kuanzia leo (jana) wimbo wetu unakuwa ni tume huru mpaka tupate tume huru ya uchaguzi,” alisemaMnyika.
“Hivyo, kama itafikia hadi Bunge linaanza Januri 28, kukiwa bado hakuna mswaada wowote kwa hati ya dharura ya marekebisho manne ya Katiba ambayo ni tume huru ya uchaguzi, kuruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani, mgombea wa urais kuzidi asilimia 50 ya kura tofauti na sasa na mgombea anayepita peke yake kupigiwa kura ya ndiyo na hapana badala ya kupita bila kupingwa kama ilivyo sasa.
“Hayo yanahitajika ni lazima wabunge wetu wafuatilie kama kuna muswada kama huu na kama serikali haitafanya hivyo basi wabunge wa upinzani waungane watengeneze mswaada na waupeleke bungeni na kitakachotokea tutawaeleza Watanzania,” alisema Mnyika.
Kuhusu kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk. Bashiru Ally, ya kusema kwamba chama hicho kinashinda kwa kuwa kina wapiga kura wa kutosha, Mnyika alisema kuwa wao wanawanachama wa kuwachagua wa kutosha lakini wamekuwa wakiangushwa kutokana na kukosekana kwa tume huru.
“Sisi tunawapiga kura wa kutosha ndiyo maana CCM wao wamekuwa wakitumia watendaji wa manispaa kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana kuengua wagombea wote wa chadema kwenye mitaa mbalimbali nchini.
“Tayari, Mkutano Mkuu wa chama uliazimia kwamba tusitoe ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaa waliopandikizwa katika maeneo mbalimbali, sasa nitoe agizo kwa chama kwamba ili tusitoe ushirikiano mkutano mkuu uliazimia kuwatangaza wale viongozi waliokuwa wameteuliwa na chama kugombea serikali za mitaa ndiyo watakuwa serikali vivuli kwenye mitaa mbalimbali.
“Kwa hiyo vikao vianze ili kuweka mikakati ya kyuonyesha kwamba sisis tuna watu na wao wana dola mna tutawashinda,” alisema