25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mnyeti: Stendi ya mabasi Babati haitarudi mjini

Beatrice Mosses, Manyara  

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewataka wananchi wa mkoa huo kufuta kwenye akili zao mawazo ya kurudisha stendi ya mabasi Babati mjini akisema ili mji wa Babati uweze kubadilika na kutanuka ni lazima kutoka nje kwani kuendelea kukaa katikati ya mji maeneo mengine hayataendelezwa.

Mnyeti ameyasema hayo alipotembelea kuangalia miundombinu ya umeme stendi mpya ya mabasi iliyopo eneo la makatanini kilomita tano kutoka eneo ilipokuwepo stendi ya zamani.

“Ninataka niwahakikishie stendi haiwezi kuhama, hapa kuna wafanyabiashara wahuni wachache wenye maduka makubwa kule mjini wanadhani kila serikali ni ya kutekenya tekenya maamuzi yanabadilika wafikishieni salamu hizi stendi hapa ndo imefika cha msingi ni kuiboresha.

“Kuna wengine wamejipanga sijui wataenda kusema wapi, nataka niwaambie kila kona nimeshaziba stendi imeshafika mahala pake hapa cha msingi ni kuboresha miundombinu na ndani ya muda mfupi itakuwa rafiki na mtaendelea na shughuli zenu,” amesema Mnyeti.

Mmoja wa wafanyabiashara waliopo stendi walimuomba RC Mnyeti awasaidie kuona namna ya kupunguziwa bei ya vibanda vyilivyopo katika eneo hilo kwani wanalipa Sh 90,000 na kwamba wangetamani wapunguziwe angalau ifike Sh 50,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles